Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu amekutana na kufanya
mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Kichina (CHINA QIYUAN
ENGINEERING CORPORATION) ambayo inatarajia kusimamia ujenzi wa Chuo cha Ufundi
Stadi, VETA cha Mkoa wa KAGERA.
Mazungumzo hayo yamefanyika
leo katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo UDOM mkoani Dodoma ambapo kwa pamoja
wamejadiliana hatua za awali za Ujenzi wa chuo hicho na kuwa tayari kampuni
hiyo imekwisha andaa michoro ya namna chuo hicho kitakavyokuwa huku
wakisisitiza kuwa ujenzi huo utafanyika kwa awamu mbili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu akifanya majadiliano kuhusu
ujenzi wa VETA mkoani KAGERA
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu
Msaidizi wa kamapuni hiyo Fang Kefang amemweleza Dk. Semakafu kuwa awamu ya
kwanza ya ujenzi huo itachukua miezi 18 na majengo yatakayojengwa yatakuwa na
uwezo wa kuchukua wanafunzi mia nne (400).
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu
akizungumza na Meneja Mkuu Msaidizi wa Idara ya Usanifu Majengo wa Kampuni ya
Ujenzi ya Kichina (CHINA QIYUAN ENGINEERING CORPORATION) Fang Kefeng, Kampuni
inayotarajiwa kusimamia ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi, VETA cha Mkoa wa
Kagera.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.