Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknlojia Profesa Joyce Ndalichako amelitaka shirikisho la Mameneja na Wamiliki
wa Shule nchini –TAMONGSCO kuwa na mtazamo chanya wanapotekekeleza majukumu yao
ikiwa ni pamoja na kuelewa kuwa kila Jambo linautaratibu wake katika
kulitekeleza.
Waziri Ndalichako ameyasema
hayo leo mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo ambapo
amesisitiza kuwa Elimu ni kitu muhimu na hakiwezi kuendeshwa bila kufuata
utaratibu, kusisitiza kuwa hata uendeshaji wa shule una taratibu zake.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mameneja na Wamiliki wa shule (TAMONGSCO) uliofanyika Mjini
Dodoma .
Profesa Ndalichako
aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa Serikali haiwezi kuweka vikwazo na
vizuizi kwa wadau wake wa Elimu, kwa kuwa lengo ni kuhakikisha Elimu bora inatolewa
kwa manufaa ya Taifa.
“Hata siku moja Serikali
haiwezi kuweka vikwazo na vizuizi kwa wadau ambao kwa namna moja ama nyingine
wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono
juhudi zinazofanywa na serikali, Pia Serikali inatambua thamani na
mchango unaotolewa na sekta binafsi katika Elimu,
“Hivyo sioni kuwa ni sahihi kwenu nyinyi TAMONGSCO kuja na
kauli mbiu inayosema kuwa “ Kwa nini
vikwazo na vizuizi katika shule na Taasisi zisizo za Serikali,”alisema Waziri
Ndalichako.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mameneja na Wamilki wa Shule (TAMONGSCO)
wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako ambaye hayupo pichani wakati akifungua Mkutano
huo.
Waziri Ndalichako pia amewataka
Mameneja na Wamiliki hao wa shule kuwa wazalendo kwa kutoa kipaumbele katika
kuajiri walimu wa Kitanzania, kabla ya kufikiria wageni.
Amesema ili kuunga mkono
kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda ni vyema
wawekezaji wakawekeza zaidi kwenye eneo la ufundi stadi, ikiwa ni pamoja na
mafunzo yanayotolewa kuendana na soko la ajira.
Kwa upande wao TAMONGSCO
wameeleza kuwa lengo la mkutano wao ni kujadiliana kwa pamoja mafanikio na
changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya Elimu ili kuzipatia ufumbuzi wa
pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.