Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu amezitaka Shule za
Sekondari nchini ambazo zimekuwa zikishindwa katika mashindano ya insha za Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika
SADC kujifunza kupitia shule ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.
Dkt. Semakafu ameyasema hayo mjini Dodoma wa
wakati hafla ya kuwazawadia washindi wa insha hizo kwa mwaka 2017 ambapo
amesema ni vema kukawa na utaratibu wa
kuzikutanisha shule hizo mara moja kwa mwaka ili kujadiliana mbinu mbalimbali
zitakazowawezesha kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Semakafu amesema ushindi huu
ni dhahiri kuwa Elimu inayotolewa nchini ni Elimu bora na diyo maana wanafunzi wa
kitanzania wameweza kushinda tuzo na kuongoza katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
na Nchi za kusini mwa Afrika.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu akimkabidhi
zawadi ya fedha mshindi wa Jumla wa Insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Michael Msafiri kutoka Shule ya Sekondari Kibaha iliyopo Mkoni Pwani.
Afisa Elimu Mkuu wa
sekretaieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki James Otieno kauli aliunga
mkono kauli hiyo kwa kusema kuwa Elimu nchini
Tanzania ni bora kwa Nchi za ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwasababu
wanafunzi kutoka Tanzania wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano hayo.
Kwa upande wake Mwanafunzi
bora wa mashindano ya insha hizo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Michael
Msafiri kutoka Shule ya Sekondari Kibaha ndiye atakuwa mwakilishi wa washindi
wote katika Mkutano Mkuu wa Wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo utakaofanyika baadae
mwaka huu mkoani Arusha.
Kaimu Mratibu wa mashindano hayo Salum
Salum kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema mshindano haya
huanza mara baada ya kikao cha wakuu wa Nchi wanachama kutoa azimio la mwaka na
kwamba mada zinazoshindanishwa huzingatia makubaliano ya wakuu wa nchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu akikabidhi zawadi kwa
mwanafunzi Anord Matungwa kutoka shule ya Sekondari Kagemu mkoani Kagera
aliyeshinda kutoka kundi la shule zenye mazingira magumu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.