Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo amezindua Jengo la
kufundishia la ghorofa 10 katika Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam- DIT – Teaching Tower Complex.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea na kukagua jengo hilo amesema kuzinduliwa kwa jengo
hilo kutasaidia kuongeza udahili wa wanafunzi kwa kuwa jengo hilo linauwezo wa
kuchukua wanafunzi zaidia ya Mia Tisa kwa mara moja.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako azindua Jengo la ghorofa
10 DIT na ameitaka Taasisi hiyo kutunza miundombinu kwa kuwa imejengwa kwa
gharama kubwa na fedha zilizotumika ni za ndani.
Ndalichako
amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuondoa upungufu wa kero
ya Miundombinu iliyokuwa inaikabili DIT kwa muda mrefu ambapo jengo hilo
limeigharimu Serikali zaidi ya Bilioni Tisa ambazo ni fedha za ndani.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na watendaji pamoja na wanafunzi wa Taasisi
ya Teknolojia Dar es Salaam(hawapo pichani) wakati wa kuzindua Jengo la kufundishia la ghorofa 10.
Kwa upande wake Mkuu wa
chuo cha DIT Profesa Preskedis Ndomba ameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo uliofanywa na Serikali ambapo amemhakikishia
Waziri wa Elimu kuwa watailinda
miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu kwa lengo la kuongeza tija
ya kuwepo kwa wataalamu wa fani mbalimbali hapa nchini
Baadhi
ya Watumishi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam –DIT -wakisikiliza kwa
makini hotuba ya Prof Joyce Ndalichako wakati wa kuzindua Jengo la kufundishia
la ghorofa 10
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.