Serikali imehaidi kuendelea kushirikiana na wadau wa Sekta ya Elimu katika kuhakikisha
watoto wa kitanzania wanapata Elimu iliyo bora ili kufikia malengo ya mkakati wa
kuwa na uchumi wa viwanda.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Wiliam Ole Nasha jijini Dar es Salaam katika kikao
cha pamoja kilichowakutanisha Wadau wa Elimu walio chini ya Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza-DFID
Naibu
Waziri Ole Nasha amesema ushirikiano wa serikali ambao umekuwepo kwa muda mrefu
na wadau hao wa Elimu umechangia katika kuhakikisha mtoto wa Kitanzania anapata
Elimu iliyo bora.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akizungumza na wajumbe katika
kikao kilichoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza-DFID.
Kikao hicho kimewashirikisha wadau wa Elimu kutoka EQUIP –T, EP4R, HDIF,GPE,
British Council, GPE, na RISE
“Elimu
bora kwa kila mtoto wa kitanzania ndiyo msimamo wa Serikali, katika kutekeleza hilo
sera ya Elimu bila malipo imekuwa na
baadhi ya chagamoto na katika
kukabiliana nazo ndiyo maana wamekuwepo wadau wa Elimu ambapo sasa wanafanya
kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kutimiza malengo yanayokusudiwa, kwani hatuwezi
kuboresha Elimu kama kila mtu atafanya kazi peke yake, Umoja ni Nguvu.”amesema
Mheshimiwa Ole Nasha.
Ole Nasha amesema mpaka sasa
wadau hao wa Elimu kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) wameshatoa kiasi cha zaidi ya bilioni 200 ambazo
zimekusudiwa kufanya uboreshaji wa Miundombinu ya shule za msingi na Sekondari,
pamoja na kukarabati na kujenga vyuo vya Ualimu.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akishiriki katika moja
ya majadiliano ya pamoja katika kikao kilichoandaliwa na Shirika la Maendeleo
ya Kimataifa ya Uingereza-DFID kikao ambacho kimefanyika
jijini Dar es salaam.
Naye
Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza-DFID Jane Miller ameishukuru
serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata katika
kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika kama zilivyokusdiwa. Kikao hicho kimewashirikisha
wadau wa Elimu kutoka EQUIP –T, EP4R,HDIF,GPE, British Council, GPE, na RISE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.