Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo amewataka Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
vya Serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafuate taratibu wakati
wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi ikiwa ni pamoja na kushirikisha watumishi
na wanafunzi wa Chuo taarifa za mapato na matumizi ya fedha.
Dk. Akwilapo ameyasema hayo leo
Jijini Dodoma wakati alipokutana na Wakuuu wa Vyuo hivyo kwa lengo la kujadili
mafanikio, changamoto na mikakati waliyonayo katika kuhakikisha majukumu na
uendeshaji wa vyuo yanatekelezeka bila changamoto ili waweze kufikia azma ya
kuandaa walimu bora.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard
Akwilapo akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali (hawapo pichani)
katika kikao kazi cha kujadili mafanikio, changamoto na Mikakati bora ya
kuwezesha Vyuo kutekeleza majukumu yake
bila changamoto Mkoani Dodoma.
Pia Katibu Mkuu huyo amewataka Wakuu wa Vyuo kuwasirikisha
wale wanaowasimamia katika kuandaa mikakati ya utendaji ili waweze kutoa
mchango katika kutekeleza mikakati hiyo na kufikia malengo mapana ya Wizara
ambayo ni kutoa Elimu bora.
Katika hatua nyingine Dk.
Akwilapo amewataka Wakuu wa Vyuo hao kuanisha mahitaji ya rasilimali watu
ambayo inahitajika vyuoni inayoendana na kozi zinazofundishwa katika Chuo
husika ili kuepuka kuwa na rasilimaliwatu isiyoendana na mahitaji ya Chuo.
Baadhi ya Wakuu wa Vyuo wakifuatilia maelekezo ya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo wakati
wa kikao cha pamoja kilichofanyika leo Agosti 31, 2018 katika Chuo Kikuu cha Dodoma
Jijini Dodoma.
Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa
Vyuo vya Ualimu vya Serikali ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu Morogoro
Agustine Sahili amesema wanaishukuru Wizara kwa kuandaa vikao vya aina hiyo
kwani vinawasaidia kuwakumbishia taratibu za kazi na kuahidi kutekeleza yale
yote waliyoagizwa ili kuimarisha utendaji katika maeneo ya kazi.
Kikao kazi hicho kimeshirikisha
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali 35 vilivyopo hapa nchini.
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali wakiwa katika
picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.
Leonard Akwilapo
Kwakweli hilo la mapato na matumizi ni ugonjwa kwa vyuo vingi
JibuFuta