- Lengo la Bodi ni kuwa na Muundo
na Chombo Cha Kisheria ili kutambua rasmi taaluma ya Ualimu kama zilivyo
taaluma nyingine
- Ili kutimiza malengo
yaliyowekwa na Serikali katika Elimu, thamani ya walimu ni jambo ambalo
linapewa kipaumbele sana.
-Muswada wa Sheria ya bodi ya
kitaalamu ya walimu umekuwa shirikishi katika hatua zote ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha Walimu,Maafisa Elimu wa Wilaya, Mikoa,Wathibiti Ubora,Chama Cha
Walimu Tanzania,Taasisi mbalimbali na Wizara ikiwemo ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).
- Wadau wengine walioshirikishwa
Kuanzia hatua za awali ni pamoja na Haki Elimu, CHAKAMWAKA, TAPIE, TAMONGSCO na
Mtandao wa Elimu Tanzania(TEN/MET)
- Malengo ya Bodi hii ya walimu
hayafanani na chombo kingine, vyama vingine vinaangalia maslahi ya walimu
wakati bodi inaenda kuleta hadhi kwa kutambua walimu wote waliopo na
wasiokuwepo madarasani.
-Tume ya Utumishi wa walimu
imejikita katika utumishi kwa maana ya kuangalia orodha ya walimu walioajiriwa
na serikali na uratibu wa masomo wakati bodi itaangalia mabadiliko mbalimbali
katika dunia ikiwa ni pamoja na kuangalia nafasi za kuwaendeleza walimu.
-Bodi pia itasimamia vigezo kwa
kuhakikisha mwalimu lazima awe amehitimu katika Chuo kinachotoa mafunzo, pia
bodi itasimamia suala la maadili kwa walimu.
-Bodi ya kitaalamu ya walimu
itakuwa na jukumu la kupokea malalamiko, kuchambua na kuyapatia ufumbuzi
malalamiko ya Walimu wachache ambao wamekuwa wakifanya matendo ambayo ni
kinyume na maadili ya Ualimu.
-Bodi itatoa fursa kwa walimu
kujadili kwa kina masuala yao ya kitaalamu kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi.
-Waziri Ndalichako pia amelaani
vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya walimu vya kutoa adhabu kwa wanafunzi
na ameonya walimu kuacha kumalizia hasira zao kwa wanafunzi.
-Waziri amesema uchapaji
hovyo wa viboko kwa wanafunzi ni kinyume na taratibu za Wizara, sasa
kuwepo kwa Bodi ya kitaalamu itahakikisha inawabana walimu watakaokwenda
kinyume na taratibu.
- Waziri amewataka walimu kuacha
mara moja tabia za kuchapa wanafunzi hovyo na badala yake wawapende watoto na
wahakikishe wanawasidia katika kuwakuza kwenye maadili na malezi yanayokubalika
kwenye Taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.