Serikali
imesema inatarajia kutoa mwongozo wa utaratibu wa kusambaza kompyuta na vifaa
vyake katika shule za msingi na sekondari ili kuwezesha vifaa hivyo kutambuliwa
ikiwa ni pamoja na kuwa na takwimu sahihi
kwa shule ambazo zitakuwa
zimepatiwa vifaa hivyo.
Kauli
hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. James Mdoe jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya
TEHAMA yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo amesema
kwa sasa ni vigumu kwa serikali kujua ni shule ngapi zenye kompyuta ama taasisi
zinazotoa misaada ya kompyuta shuleni.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza na washiriki wa mafunzo ya TEHAMA
(hawapo Pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam ambapo
amewataka washiriki hao kutumia maarifawaliyoyapata katika kuboresha Elimu
“Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakaa pamoja na Ofisi ya Rais Tawalaza Mikoa
na Serikali za Mitaa ili tuweze kuweka mwongozo ambao utawezesha serikali
kutambua taasisi zote zinazojishughulisha na usambazaji wa kompyu takatika
shule pamoja na kutambua shule zilizo na kompyuta ili iwe rahisi
kuziratibu”amesema Prof. Mdoe.
Akizungumza
na Walimu walioshiriki mafunzo hayo amewataka kuhakikisha wanatumia maarifa waliyoyapata katika kuboresha elimu
na kuimarisha utendaji wa kazi ili kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini.
Kwa
upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Pius Joseph amesema mfuko wa
Mawasiliano kwa wote ina jukumu la
kuhakikisha ina ziunganisha shule zote za msingi na sekondari katika
mtandao wa inteneti, pamoja na kutoa vifaa na mafunzo kwa walimu wanaofundisha
masomo ya TEHAMA .
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akimkabidhi cheti cha kumaliza
mafunzo ya TEHAMA mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar
es Salaam.
Mfuko huo wa Mawasiliano tayari umetoa mafunzo yaTEHAMA kwa walimu 578 kutoka mikoa yote ya Tanzania pia
umetoa kompyuta 425 kwa shule za msingi,
komputa 1250 kwa shule za sekondari
na kuwa vifaa hivyo vimetolewa katika
kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.