Serikali
imevitaka vyuo vyote vya Elimu ya Juu nchini kuzingatia kanuni na miongozo inayotolewa na Baraza la Taifa la Ufundi
(NACTE) na Tume ya vyuo Vikuu Nchini
(TCU) katika kutoa elimu ili kuepuka kufungiwa au kufutiwa udahili.
Kauli
hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa
Elimu, Sayansi naTeknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika mahafali ya 53 ya Chuo
cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam, ambapo amesema serikali
kupitia TCU na NACTE itaendelea kusimamia ubora wa Elimu na kuvifungia vyuo
vyote vinavyotoa elimu chini ya kiwango.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika maandamano
ya kitaaluma wakati wa mahafali ya chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya
Dar es Salaam.
Waziri
Ndalichako amesema kuna baadhi ya Vyuo ambavyo vimekuwa havifuati taratibu na
miongozo inayotolewa na TCU na NACTE na kusababisha usumbufu kwa wanafunzi pale
vinapotakiwa kufungiwa, na kusisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa na Taasisi
hizo ni endelevu na kuwa lengo ni
kuhakikisha wahitimu wanapata Elimu bora itakayowawezesha kujiajiri ama kuajiriwa.
Waziri Ndalichako pia amewataka Wahadhiri
wenye tabia yakuficha matokeo ya wanafunzi kwa madai ya kukosa maslahi yao
kutoka kwa mwajiri kuacha mara moja
tabia hiyo kwani imekuwa ikiwasumbua wanafunzi ambao hawana hatia.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wahitimu
katika mahafali ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam
amewataka kuwa wanafunzi kuwa mabalozi wazuri na wazalendo katika kazi zao
baada ya kuajiriwa ama kujiajiri.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo Cha CBE Prof. Emanuel Mjema amesema chuo hicho
kinakabiliwa na changamoto ya uvhakavu wa miundombinu kutokana na Chuo hicho
kuwa cha muda mrefu, hivyo Marion a serikali kukipatia udhamini
ili kiweze kukopa katika Taasisi za fedha ili kuboresha miundombinu hiyo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimbalisha mmoja wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Maendeleo katika mahafali ya Chuo cha
Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.