Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana
Dkt. Filisi Nyimbi amesema serikali ya awamu ya tano imeweka misingi imara
itakayowezesha kila mtanzania kupata elimu iliyo bora na yenye tija kwa Taifa
ili kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo mwaka
2025.
Ameyasema hayo wakati akifungua
mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoojia
unaofanyika mkoani Mwanza na kusisitiza kuwa Wizara hiyo imepewa jukumu la
kutunga sera, kuandaa na kusimamia miongozo mbali mbali ya Elimu itakayowezesha
Elimu inayotolewa nchini kuwa bora.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa wameshikana
mikono wakati wa kiimba wimbo wa “SOLIDARIRY” kuashiria umoja, mshikamano na
upendo katika utekelezaji wa majukumu yao
Dkt. Nyimbi amesisitiza kuwa
ili kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano kila mtumishi ana wajibu wa kufanya
kazi kwa bidii na kwa weledi wa hali ya juu.
Dkt. Nyimbi ameipongeza
Wizara ya Elimu kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na
kufundishia katika Shule za Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Elimu ya Juu, Vyuo vya
Ufundi, na Vyuo vya Maendeleo ya
wananchi (FDCs) lengo likiwa ni kuweka mazingira bora ya kielimu katika kuandaa
vijana wenye sifa katika kujenga uchumi wa nchi.
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Filisi Nyimbi Akizungumza na washiriki katika Mkutano
wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia ambapo watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa weledi kwa
kuzingatia kanuni, taratibu na sheria.
Pia ameipongeza Wizara kwa
kuendelea kuimarisha na kuboresha idara
ya Uthibiti Ubora wa shule kwa kununua magari ili idara hiyo iendelee kukagua
shule na kutoa ushauri wa kitaalamu na
kitaaluma.
Akizungumza katika mkutano
huo Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe amesema pamoja na mambo mengine kikao
hicho kitapitia utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2018/19 na kujadili mwelekeo wa
bajeti kwa mwaka 2019/20.
Mgeni
rasmi Dkt. Filisi Nyimbi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
na washiriki wa Mkutano wa 20 wa Baraza
la Wafanyakazi wakiwa kwenye picha ya pamoja. Kikao kazi hicho kimefanyikia
mkoani Mwanza.
“Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia imeendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa majukumu yake kwa
lengo la kuboresha sekta ya Elimu hapa nchini, hivyo niwaase watendaji wote
kuendelea kufanya kazi kwa kufauta kanuni, taratibu na sheria zinazosimamia
utendaji katika maeneo yenu ya kazi,”alisisitiza Prof. Mdoe.
Mkutano huu umehudhuriwa na
wajumbe zaidi ya 120 kutoka Wizara ya Elimu na wajumbe kutoka Chama cha Walimu
Tanzania ( CWT ) na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE). Kauli mbiu ya Mkutano huo wa 26 wa baraza la
wafanyakazi ni: “Elimu bora na Uwajibikaji wa pamoja ni Chachu ya Maendeleo ya
Uchumi wa Viwanda Tanzania”
Baadhi ya washiriki wa Mkutano
wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo
unaofanyika Jijini Mwanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.