Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Romania Daniela Gitman pamoja na ujumbe wa Kamati
ya Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Romania na kukubaliana kushirikiana katika
sekta ya elimu.
Akizungumza
na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Ndalichako jijini Dodoma,
Balozi Gitman amesema hii ni mara ya
kwanza kwa nchi yake kuingia katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa lengo la
kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Balozi
Gitman amesema nchi yake imeiteua Tanzania kuwa chimbuko la kuanzishwa kwa ushirikiano kati Serikali ya Romania na nchi
za Afrika Mashariki kwenye maeneo mbalimbali ambapo wanaanza na sekta ya elimu
na baadaye wataaangalia sekta za utalii na biashara.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Katibu Mkuu Prof.
Prof. James Mdoe, Kaimu Mkurgenzi Elimu ya Juu na Mkurugenzi wa Sayansi,
Teknolojia na Ubunifu Dkt. Kipanyula wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Heshima kutoka Romania na Wajumbe
wengine.
Katika
Kikao hicho wamekubaliana kutoa ufadhili wa masomo ya shahada za juu kwa
wahadhiri na wataalamu katika Vyuo Vikuu vya Tanzania katika fani ambazo Umoja
wa Wakuu wa Vyuo Vikuu Tanzania utapendekeza kulingana na vipaumbele vya nchi.
Pamoja
na kufadhili wahadhiri, Wamekubaliana kupitia Vyuo Vikuu kuanza utaratibu wa
kubadilishana uzoefu na utaalamu “fellowships”, ambapo wahadhiri kutoka
Tanzania wataenda Romania na Romania kuja Tanzania kwa vipindi vifupi vifupi.
Waziri
Ndalichako ameishukuru serikali ya Romania na kuahhidi kushirikiana nao katika
kuendeleza sekta ya elimu na kuuwataka Umoja wa Wakuu wa Vyuo Vikuu nchini
kuhakikisha wanakamilisha kuandaa makubaliano ya ushirikiano huo pamoja na taratibu
za utekelezaji wa ushirikiano huo.
Katika
hatua nyingine Romania imetoa fursa ya kufadhili masomo ya Elimu ya Juu kwa
wanafunzi 5 katika kila fani itakayopendekezwa kusoma katika Vyuo Vikuu nchini
humo. Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na vyuo vikuu wataratibu upatikanaji wa
wanufaika.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. James Mdoe na Mkurugenzi wa Elimu Juu
Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia na Wakurugenzi wa Wizara hiyo ambapo
utakelezaji wa makubaliano hayo unatarajiwa kuanza mara baada ya kusaini
makubaliano ya ushirikiano na programu za maunzi kwa wanufaika zinatarajiwa
kuanza mwezi Oktoba Mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.