Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameipongeza Jamhuri ya Watu
wa China kwa kuimarisha ushirikiano na Tanzania hususan katika
sekta za Elimu, Biashara na Ujenzi wa miundombinu.
Waziri Ndalichako
ametoa pongezi hizo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa
Kidiplomasia kati ya Tanzania na China ambapo amesema kuwa
mahusiano kati ya nchi hizo mbili ni
ya muda mrefu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce
Ndalichako
akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia
kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Prof.
Ndalichako amesema mchango wa nchi hiyo kwenye maendeleo ya
Tanzania ni dhahiri akitolea mfano wa ujenzi wa Reli ya TAZARA pamoja na
ujenzi wa viwanda mbalimbali vya nguo nchini.
Prof. Ndalichako amesema pia China imeendelea
kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa kubadilishana uzoefu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Wag Ke (Hayupo pichani) katika sherehe za kuadhimisha
miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Tanzania.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu,
Mhe. Mizengo Pinda, Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara, na viongozi mbalimbali kutoka
Taasisi za umma na binafsi nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.