Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (Mb) amezindua
machapisho ya kitaaluma yaliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam
ambapo amesema kwa muda mrefu machapisho ya kitaaluma yamekua yakiandikwa kwa
lugha ya Kiingereza na kupelekea watanzania wengi kutopata majibu ya tafiti
zinazofanywa na wanataaluma hao.
Waziri
Ndalichako amewapongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa hatua hiyo kubwa
ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuhakikisha maarifa
yanawafikia wananchi wote hasa katika kipindi hiki ambapo nchi inapoelekea uchumi
wa kati kupitia viwanda.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizindua machapisho ya Kitaaluma
yaiandikwa kwa lugha ya Kiswahili, uzinduzi huo umefanyika katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.
"Nawapongeza wanataaluma kwa kutoa machapisho ya tafiti zao kwa kutumia Lugha Adhimu ya Kiswahili endeleeni kufanya tafiti zaidi kwa maendeleo ya nchi," amesema Ndalichako.
Akimkaribisha
Waziri kuzindua machapisho hayo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.
William Anangisye amempongeza Waziri kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia elimu
nchini.
Prof.
Anangisye amesisitiza kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitaendeleza kazi yake
muhimu ya utafiti kwa ubora wa hali ya juu na kutoa machapisho katika majarida
ya kitaaluma yenye hadhi ya juu ya kimataifa na kitaifa.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akionyesha moja ya Chapisho mara
baada ya kuzindua machapisho ya Kitaaluma yaiandikwa kwa lugha ya Kiswahili,
uzinduzi huo umefanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijini Dar es
Salaam
Akiongea
kwa niaba ya waandishi wa machapisho mbalimbali ya tafiti Eliah amekishukuru
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kumuwezesha kuandika kitabu kinachohusu
Matumizi ya Kiswahili katika Vyombo vya Habari ikiwa ni juhudi za kuhakikisha jamii inapata kazi
za waandishi wa habari katika umahiri wa hali ya juu.
Nae
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Bonaventure Rutinwa
amewataka wananchi kununua na kusoma vitabu mbalimbali ili kujichotea maarifa na
kujiendeleza katika lugha hasa ya Kiswahili kwa sababu ina fursa nyingi sana za
ajira ndani na nje ya nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.