Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewaasa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Iringa kutumia mfumo
wa elimu kuandaa vijana ambao watakuwa na mtazamo chanya na mawazo ya kimaendeleo yanayolenga kuja na majawabu ya changamoto
mbalimbali zinazojitokeza katika jamii, ametaka vijana wajengwe katika kuona
fursa zaidi.
Amesema hayo katika siku ya maadhimisho
ya Kitivo cha Sayansi na Elimu katika Chuo Kikuu cha Iringa ambapo alikuwa Mgeni Rasmi katika siku hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka mkoani Iringa.
Ndalichako amewataka vijana wanaosoma katika Chuo hicho kusoma kwa bidii
ili elimu wanayoipata iweze kuwasaidia
wao binafsi na jamii zinazowazunguka.
“Serikali yenu sikivu inaendelea
kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati na kuboresha elimu nchini, kwa hili
tumpongeze Rais wetu, na kama kauli mbiu ya hapa kazi inavyosema, Rais na sisi tunachapa kazi
ninyi kazi yenu ni kusoma kwa bidii ili mkimaliza muweze kushiriki moja
kwa moja katika kujenga uchumi katika taifa letu.”
Ndalichako amesema Serikali inaendelea kuboresha mifumo ya usimamizi wa elimu ya juu kupitia Tume ya Vyuo Vikuu kwa lengo la kuhakikisha Vyuo vinatoa wahitimu bora na wenye sifa na ujuzi kwa ajili ya kuajiriwa na vile vile wenye ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na amewataka Uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kasoro zilizotolewa na TCU katika baadhi ya programu zao ambazo zimesitishwa zinarekebishwa kwa haraka ili zipate ithibati. Ametumia nafasi hiyo pia kuwataka Vyuo Vikuu nchini kufuata Kanuni, Sheria na taratibu za uendeshajI Vyuo wakati wote.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu Iringa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kitivo cha Sayansi na Elimu katika Chuo Kikuu cha hicho. |
Ndalichako amesema Serikali inaendelea kuboresha mifumo ya usimamizi wa elimu ya juu kupitia Tume ya Vyuo Vikuu kwa lengo la kuhakikisha Vyuo vinatoa wahitimu bora na wenye sifa na ujuzi kwa ajili ya kuajiriwa na vile vile wenye ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na amewataka Uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kasoro zilizotolewa na TCU katika baadhi ya programu zao ambazo zimesitishwa zinarekebishwa kwa haraka ili zipate ithibati. Ametumia nafasi hiyo pia kuwataka Vyuo Vikuu nchini kufuata Kanuni, Sheria na taratibu za uendeshajI Vyuo wakati wote.
Akiwa chuoni hapo ameongezea kuwa Serikali
inathamini mchango wa sekta binafsi katika kutoa elimu huku akitolea mfano
uwekezaji uliofanywa katika Chuo hicho na Serikali kwa kutoa mitambo na vifaa mbalimbali vya Tehama vinavyowezesha
utumiaji wa mkongo wa Taifa.
Awali akitembelea kituo atamizi cha
chuo hicho, amepongeza juhudi mbalimbali zilizofanyika katika kituo hicho kwa
kulea mawazo ya kibunifu hadi kufikia kutayarisha bidhaa, kuanzishwa biashara na
kutoa mafunzo ya ujasiriamali na masoko kwa wanachuo na jamii inayowazunguka.
Aidha amewataka vijana waliobuni bidhaa kuhakikisha wanafuata taratibu za kurasimisha bidhaa zao.
Waziri Ndalichako amefurahishwa na
uwezo mkubwa waliyouonesha wanafunzi wabunifu walio katika kituo hicho na
kuwataka kuendelea na mawazo na mtazamo wa kijasiriamali ambapo amesema hayo ni
matokeo halisi ya mafunzo yanayotolewa na chuo hicho katika Shahada ya Ujasiriamali na Masoko kwa vitendo yaani “Bachelor of Applied Marketing and Entrepreneurship.”
Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Makamu Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Iringa kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania Prof. Ndelerio Urio, amesema
mwaka huu chuo kina wanafunzi zaidi ya 3,215. Amemshukuru Waziri kwa kutembelea
Chuo hicho na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kusaidia vyuo binafsi. Prof
Urio ameahidi kuendelea kusimamia ubora
katika utoaji elimu ili kuendelea kutoa wahitimu bora akisistiza kuwa
wataendelea kujitathmini kila wakati ili kuhakikisha wanakuwa na programu bunifu
zinazokidhi mahitaji ya soko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.