Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na ile ya
kufundishia lengo likiwa ni kuhakikisha Elimu bora inatolewa.
Waziri Ndalichako ameyasema
hayo wakati akifungua vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa
Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) katika
Shule ya Msingi Mahembe iliyopo Kijiji cha Mahembe kata ya Sawida mkoani Simiyu
Kupitia ziara hiyo Profesa Ndalichako pia alizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Habiya kilichopo
Wilaya ya Itilima na kuwataka wazazi kuhakikisha watoto wote waliofika umri
wa kwenda shule wanakwenda.
Kwa upande wake Mbunge wa
Jimbo la Itilima, Mkoani Simiyu Njalu Silanga amepongeza jitihada zinazofanywa
na Serikali za kuboresha miundombinu huku akiwataka wananchi wa Jimbo lake
kuitunza miundombinu hiyo kwa faida ya kijiji
hicho.