Zaidi
ya shilingi milioni Mia moja zimepatikana wakati wa Harambee ya Ujenzi wa
mabweni ya wasichana katika shule ya
sekondari Sovi iliyopo kata ya Mtwango
Mkoani Njombe.
fedha
hizo zimepatikana wakati wa harambee
iliyoongozwa na Waziri wa Elimu, Sayasni na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako mwishoni mwa wiki mkoani Njombe ambapo amewataka vijana kuwa wazalendo, pamoja na kuhakikisha
wanasoma kwa bidii kwa maslahi ya Taifa.
Waziri
Ndalichako pia amewasihi vijana
kuhakikisha wanaipenda nchi yao pamoja na kujiepusha na makundi ambayo hayana
tija kama vile utumiaji wa dawa za kulevya, kujiingiza kwenye makundi ya
uhalifu, na utumiaji wa pombe vitendo ambavyo havina faida kwa maisha yao ya
sasa na ya baadae.
Waziri
Ndalichako amesema kuwepo kwa mabweni kutawapunguzia wanafunzi kutembea umbali
mrefu, kuwaepusha na vishawishi vya barabarani wakati wa kwenda na kurudi
shuleni na hivyo watatumia muda wao
mwingi kwenye kusoma.
Ndalichako
amesema kazi ya Serikali ni kuboresha miundombinu, na kuhakikisha mahitaji
muhimu ya wanafunzi yanapatikana shuleni hivyo wanafunzi nao lazima watimize
wajibu wao kwa kuhakikisha wanasoma na kufaulu katika mitihani yao.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema mkoa wake
unatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kutatua
changamoto mbalimbali katika sekta ya Elimu.
Amesema
katika mkoa wake kati ya Shule Kumi za sekondari za umma shule Tisa zina
mabweni lengo likiwa ni kuondoa changamoto ya upatikanaji wa mimba kwa wanafunzi,
pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha Nne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.