Jumatano, 22 Machi 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII IKIKAGUA JENGO LA TEACHING TOWER LILILOPO DIT.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Maendeleo na huduma za jamii wakikagua jengo la kufundishia, ambalo ndani yake kuna ofisi, chumba cha ujasiriamali, na vyumba vya madarasa, (Teaching Tower)








Jumanne, 21 Machi 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA MLOGANZILA.

Kamati ya bunge ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Maendeleo na huduma za jamii, Peter Serukamba na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Naibu waziri Mhandisi Stella Manyanya na Naibu katibu Mkuu Dkt. Leonard Akwilapo, wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua mradi wa MLOGANZILA chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).








Jumapili, 19 Machi 2017

NAIBU WAZIRI AZINDUA VISHKWAMBI.

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amewataka wadau wa Maendeleo ndani na nje ya nchi kuangazia maeneo ya vijijini kufuatia miradi mbalimbali ya maeneo kuangazia maeneo ya mijini zaidi.

Mheshimiwa Manyanya ametoa kauli hiyo hii leo katika shule ya msingi ya Olympio wakati akikabidhi vishkwambi (tablets)ambavyo vinatarajiwa kusambazwa katika shule mbalimbali za jijini Dar es salam.

Mhandisi Manyanya amesema umefika wakati sasa mradi wa majaribio kama huu wa Elimu kwa njia ya TEHAMA upelekwe hadi maeneo ya vijijini na siyo kubakia kwenye maeneo ya mijini pekee.

Naibu Waziri manyanya pia amewataka walimu kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa hasa ya kuwafundishia wanafunzi.

 





Ijumaa, 3 Machi 2017

WAZIRI WA ELIMU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA WANANCHI (FDCs).

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya wananchi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi Kwa uadilifu, ubunifu, na weledi wa hali ya juu ili vijana wanamaliza kwenye vyuo hivyo wawe na ujuzi na uwezo wa kujiajiri wenyewe.

MAMBO YA MSINGI AMBAYO WAKUU WA VYUO  VYA FDCs WAMETAKIWA KUZINGATIA;
1-KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA
2- WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU
3- WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA MSHIKOMANO
4- WAMETAKIWA KUWA WAADILIFU
5- WAMETAKIWA KUTUMIA NA KUTHAMINI RASILIMALI 






WAZIRI WA ELIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA DFID.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako jana amekutana na kufanya mazungumzo na  washirika wa Maendeleo kutoka nchini Uingereza (DFID)  mjini Dodoma ambapo Kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuboresha Miundombinu katika sekta ya Elimu
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifurahia jambo na wageni wake ambao ni washirika wa Maendeleo kutoka nchini Uingereza, DFID waliofika katika ofisi za wizara hiyo mkoani Dodoma


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na washirika wa Maendeleo DFID wa nchini Uingereza kwenye ofisi za wizara ya Elimu mkoani Dodoma ambapo Kwa pamoja wamekubaliana kuboresha miundombinu ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Waziri wa Elimu akisalimia na wageni wake kabla ya kuanza Kwa mazungumzo yao ambayo yalijikita zaidi katika masuala mbalimbali ya sekta ya Elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabweni ya wasichana Kwa wanafunzi wa vijijini  ili kuwaondolea adha wanafunzi kutembea umbali mref.



Jumatano, 1 Machi 2017

Wizara ya Elimu yahamia Dodoma


Waziri wa Elimu  sayansi na teknolojia profesa Joyce ndalichako leo ametanga za  kuwa wizara hiyo imehamia rasmi Dodoma. Viongozi wakuu wote akiwemo mhe.waziri, mhe.naibu waziri, katibu mkuu, naibu Makatibu Wakuu wote tayari wamesharipoti Dodoma katika awamu hii ya kwanza.

Mawasiliano yote yafanyike kupitia anuani ifuatayo:
Katibu mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
S.L.P. 10
DODOMA

Namba ya simu: 026- 2963633
Tovuti: www.moe.go.tz

Barua pepe: info@moe.go.tz

viongozi wa juu wa wizara wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vilivyochini ya wizara hiyo

Waziri wa Elimu profesa joyce ndalichako akitangaza kuhamia rasmi makao makuu ya nchi, Dodoma.

viongozi wa wizara, wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya wizara ya Elimu wakifuatilia maelekezo kutoka Kwa waziri wa Elimu.

Viongozi wa wizara wakikagua majengo ya ofs za wizara ya Elimu.





Jumatatu, 20 Februari 2017

Serikali za Tanzania na China zatia saini ujenzi wa Chuo cha VETA Kagera



 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi na Mwakilishi wa Masuala  ya Uchumi na Biashara ya Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong wametiliana saini makubaliano ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA kitakachojengwa  Gera mkoani kagera


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi akibadilishana hati za makubaliano (MOU) na Mwakilishi wa Masuala  ya Uchumi na Biashara wa Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong mara baada ya kutiliana saini.