Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi
Stella Manyanya akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Maendeleo na
huduma za jamii wakikagua jengo la kufundishia, ambalo ndani yake kuna ofisi,
chumba cha ujasiriamali, na vyumba vya madarasa, (Teaching Tower)
Jumatano, 22 Machi 2017
Jumanne, 21 Machi 2017
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA MLOGANZILA.
Kamati ya bunge ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Maendeleo na huduma za jamii, Peter Serukamba na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Naibu waziri Mhandisi Stella Manyanya na Naibu katibu Mkuu Dkt. Leonard Akwilapo, wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua mradi wa MLOGANZILA chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Jumapili, 19 Machi 2017
NAIBU WAZIRI AZINDUA VISHKWAMBI.
Naibu waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amewataka wadau wa Maendeleo
ndani na nje ya nchi kuangazia maeneo ya vijijini kufuatia miradi mbalimbali ya
maeneo kuangazia maeneo ya mijini zaidi.
Mheshimiwa Manyanya
ametoa kauli hiyo hii leo katika shule ya msingi ya Olympio wakati akikabidhi
vishkwambi (tablets)ambavyo vinatarajiwa kusambazwa katika shule mbalimbali za
jijini Dar es salam.
Mhandisi Manyanya
amesema umefika wakati sasa mradi wa majaribio kama huu wa Elimu kwa njia ya
TEHAMA upelekwe hadi maeneo ya vijijini na siyo kubakia kwenye maeneo ya mijini
pekee.
Ijumaa, 3 Machi 2017
WAZIRI WA ELIMU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA WANANCHI (FDCs).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya wananchi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi Kwa uadilifu, ubunifu, na weledi wa hali ya juu ili vijana wanamaliza kwenye vyuo hivyo wawe na ujuzi na uwezo wa kujiajiri wenyewe.
WAZIRI WA ELIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA DFID.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako jana amekutana na kufanya mazungumzo na washirika wa Maendeleo kutoka nchini
Uingereza (DFID) mjini Dodoma ambapo Kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza
ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuboresha Miundombinu
katika sekta ya Elimu
Jumatano, 1 Machi 2017
Wizara ya Elimu yahamia Dodoma
Waziri wa Elimu
sayansi na teknolojia profesa Joyce ndalichako leo ametanga za kuwa
wizara hiyo imehamia rasmi Dodoma. Viongozi wakuu wote akiwemo mhe.waziri,
mhe.naibu waziri, katibu mkuu, naibu Makatibu Wakuu wote tayari wamesharipoti
Dodoma katika awamu hii ya kwanza.
Mawasiliano yote
yafanyike kupitia anuani ifuatayo:
Katibu mkuu
Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia
S.L.P. 10
DODOMA
Namba ya simu: 026-
2963633
viongozi wa juu wa wizara wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vilivyochini ya wizara hiyo |
Waziri wa Elimu profesa joyce ndalichako akitangaza kuhamia rasmi makao makuu ya nchi, Dodoma. |
viongozi wa wizara, wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya wizara ya Elimu wakifuatilia maelekezo kutoka Kwa waziri wa Elimu. |
Viongozi wa wizara wakikagua majengo ya ofs za wizara ya Elimu. |
Jumatatu, 20 Februari 2017
Serikali za Tanzania na China zatia saini ujenzi wa Chuo cha VETA Kagera
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi na Mwakilishi wa Masuala ya Uchumi na Biashara ya Jamhuri ya watu wa
China nchini Tanzania Lin Zhiyong wametiliana saini makubaliano ya ujenzi wa
Chuo cha Ufundi Stadi VETA kitakachojengwa
Gera mkoani kagera
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi akibadilishana hati za
makubaliano (MOU) na Mwakilishi wa Masuala
ya Uchumi na Biashara wa Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin
Zhiyong mara baada ya kutiliana saini.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)