Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholaus Bureta akifungua maadhimisho
ya siku ya Kisomo Duniani (International Literacy Day)Kwa niaba ya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish, katika
ukumbi wa makumbusho ya Taifa. Maadhimisho haya yalienda sambamba na ufunguzi wa
ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu.
Mwakilishi wa UNESCO nchini
Bi.Zulmira Rodriguez akimkabidhi Kaimu kamishna wa Elimu ripoti ya Kimataifa ya
Ufuatiliaji wa Elimu wakati wa maadhimisho ya siku ya kisomo duniani yaliyofanyika
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Kaimu Kamishna wa Elimu Nicholaus
Bureta akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, mashirika
ya Kimataifa ya maendeleo pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali wakionyesha
ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu mara baada ya uzinduzi wake rasmi.
Kushoto mwanzoni ni Mwakilishi wa UNESCO nchini Bi.Zulmira Rodriguez.
Kaimu Kamishna wa Elimu Nicholaus
Bureta akiwakabidhi ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu baadhi ya
walimu wakuu wa shule za Msingi nchini mara baada ya uzinduzi rasmi wa ripoti
hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya kisomo duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.