Katibu mkuu wizara ya
Elimu Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi ametembelea na kukagua ujenzi
unaoendelea wa majengo ya chuo cha Veta kilichopo kihonda mkoani
Morogoro.
Katibu Mkuu Tarishi
amekagua jengo la utawala na majengo mawili ya karakana ikiwemo karakana
ya umeme wa magari na karakana ya ufundi seremala, na kuwa ujenzi wa
majengo hayo kwa hivi sasa uko katika hatua za kupauliwa.Jumatatu, 27 Machi 2017
Ijumaa, 24 Machi 2017
NAIBU KATIBU MKUU AFUNGA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard akifunga kongamano
la siku tatu la wadau wa Elimu waliokutana kuzungumzia masuala ya uongozi na
usimamizi wa masuala ya Elimu katika karne ya 21 lililofanyika katika Chuo
Kikuu cha Aga Khan, Taasisi ya kuendeleza Elimu Afrika Mashariki.
UZINDUZI WA MAKTABA.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Dkt Leonard Akwilapo akizindua maktaba ya Makumbusho ya Taifa Baada ya kupokea
vifaa vya maktaba hiyo ikiwa pamoja na vishikwambi
(TABLETS kutoka kwa Serikali ya Watu wa Korea kupitia
mradi wa THANK YOU SMALL LIBRARY.
Jumatano, 22 Machi 2017
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII IKIKAGUA JENGO LA TEACHING TOWER LILILOPO DIT.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi
Stella Manyanya akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Maendeleo na
huduma za jamii wakikagua jengo la kufundishia, ambalo ndani yake kuna ofisi,
chumba cha ujasiriamali, na vyumba vya madarasa, (Teaching Tower)
Jumanne, 21 Machi 2017
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA MLOGANZILA.
Kamati ya bunge ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Maendeleo na huduma za jamii, Peter Serukamba na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Naibu waziri Mhandisi Stella Manyanya na Naibu katibu Mkuu Dkt. Leonard Akwilapo, wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua mradi wa MLOGANZILA chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Jumapili, 19 Machi 2017
NAIBU WAZIRI AZINDUA VISHKWAMBI.
Naibu waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amewataka wadau wa Maendeleo
ndani na nje ya nchi kuangazia maeneo ya vijijini kufuatia miradi mbalimbali ya
maeneo kuangazia maeneo ya mijini zaidi.
Mheshimiwa Manyanya
ametoa kauli hiyo hii leo katika shule ya msingi ya Olympio wakati akikabidhi
vishkwambi (tablets)ambavyo vinatarajiwa kusambazwa katika shule mbalimbali za
jijini Dar es salam.
Mhandisi Manyanya
amesema umefika wakati sasa mradi wa majaribio kama huu wa Elimu kwa njia ya
TEHAMA upelekwe hadi maeneo ya vijijini na siyo kubakia kwenye maeneo ya mijini
pekee.
Ijumaa, 3 Machi 2017
WAZIRI WA ELIMU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA WANANCHI (FDCs).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya wananchi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi Kwa uadilifu, ubunifu, na weledi wa hali ya juu ili vijana wanamaliza kwenye vyuo hivyo wawe na ujuzi na uwezo wa kujiajiri wenyewe.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)