Jumatano, 11 Septemba 2019
Jumanne, 10 Septemba 2019
Jumatatu, 9 Septemba 2019
SERIKALI YATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU VYUO VYA SERIKALI
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia imetangaza sehemu ya pili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na
mafunzo ya ualimu katika vyuo 35 vya serikali.
Akitoa taarifa hiyo
jijini Dodoma mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema jumla ya wanafunzi 2,834
wamechaguliwa kujiungana mafunzo ya ualimu ambapo kati yao 1,013 ni wa
Astashahada na 1,821 ni wa Stashahada.
Dkt. Akwilapo ameongeza
kuwa hadi sasa jumla ya wanafunzi 11,028 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya
ualimu vya serikali ambapo kati yao wanafunzi 8,194 walichaguliwa awali na
TAMISEMI na 2,834 wamechaguliwa na NACTE.
Aidha, Dkt. Akwilapo
amewataka wanafunzi hao waliochaguliwa kuripoti katika vyuo walivyopangiwa
kuanzia tarehe 20 Septemba mwaka huu na kwamba mwisho wa kuripoti ni tarehe 6
Oktoba mwaka huu. Amesisitiza
wahakikishe wanaripoti ndani ya muda huo kwani baada ya hapo hawatapokelewa na
nafasi zao zitajazwa na wengine wenye sifa ambao walikosa nafasi.
“Wanafunzi wote
waliochaguliwa wanatakiwa waripoti katika vyuo vyao kuanzia tarehe 20 mwezi huu
hadi 6 Oktoba mwaka huu. Watakaoripoti baada ya hapo hawatapokelewa na
nafasi zao zitajazwa na wanafunzi wengine walioomba ambao wana sifa ila
walikosa nafasi,” amesisitiza Dkt. Akwilapo.
Aidha, Dkt. Akwilapo
amesema serikali inatambua kuwepo kwa wanafunzi wengi waliokosa nafasi za
kujiunga na masomo katika kozi mbalimbali na hivyo ameliagiza Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi (NACTE) kufungua dirisha dogo la udahili kwa siku 14 kuanzia
tarehe 7 Septemba ili wanafunzi waliokosa nafasi za masomo katika kada
mbalimbali waweze kutumia fursa hiyo.
“Wizara inatambua kuwepo
kwa idadi kubwa ya waombaji waliokosa nafasi katika awamu hii kutokana aidha na
ushindani au kutofanya uchaguzi sahihi wa kozi hivyo wizara inaiagiza NACTE
kufungua dirisha dogo la udahili kuanzia leo tarehe 7 hadi 21 Septemba ili
kuwapa nafasi waombaji waliokosa nafasi katika programu mbalimbali waweze
kufanya uchaguzi upya,” amesema Dkt. Akwilapo.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu akiongea katika
mkutano huo amesema baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakichagua kozi ambazo hawana
sifa zinazohitajika. Amewaasa waombaju kuzingatia
sifa za kozi ili kuepuka kuenguliwa kwani masharti yanayowekwa kuhusu sifa
hayabadilishwi.
“Utakuta kwa mfano mtu
ana ufaulu mzuri wa alama A hadi C katika masomo ya lugha, badala ya kuchagua
kozi zinazotaka ufaulu wa lugha yeye atachagua kozi za masomo ya sayansi ambayo
kapata alama D, matokeo yake anajikuta hachaguliwi katika kozi alizoomba,”
amesema Dkt. Semakafu.
Naye Mkuu wa Kitengo cha
Udahili wa NACTE, Twaha Twaha amewatahadharisha waombaji hasa wa kozi za afya
kuhakikisha kuwa wamefaulu vizuri katika masomo ya sayansi kwani ndio sifa ya
msingi katika udahili wa kozi hizo.
“Katika kozi za afya
vigezo vinaangalia masomo, mfano mwanafunzi anayetaka kusoma clinical medicine
au nursing, anatakiwa awe na ufaulu wa alama D katika masomo ya Physics,
Chemistry na Biology. Sifa zote hizi
zipo katika kitabu cha Mwongozo wa Udahili ambacho kinapatikana kwenye tovuti
ya NACTE ambayo ni www.nacte.go.tz,” amesema Twaha.
Alhamisi, 29 Agosti 2019
TAARIFA KWA UMMA
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY
COMMONWEALTH SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE UNITED KINGDOM 2020
The
Ministry of Education, Science, and Technology as a Nominating Agent in the
Country for the Commonwealth Scholarships is inviting applications from
qualified Tanzanians for Masters and Doctoral Degree Tenable in the United
Kingdom for the academic year 2020.
The
Scholarship includes:
- One year taught Master Degrees
- Doctoral degree of up to three years duration.
Qualification:
i.
Applicants must be holders of
bachelor or masters degrees.
ii.
Applicants for master’s degree must have a
bachelor degree with a GPA of not less than 3.5.
iii. Applicants for PhD must have a
master’s degree with a GPA of not less than 4.0.
Mode of application:
- All applications should be made directly to the Commonwealth secretariat before 30th October 2019 and should be online using the following link http://cscuk.dfid.gov.uk/apply/applicants;
- It is important that applicants should read and understand all instructions when filing the application forms, and all applicants must attach all the required attachments such as certified copies of academic certificates, transcripts, and birth certificates and submit them online through the above link;
- All applicants must ensure that, referees submit reference letter on time;
- Applicants who are employees must attach letters from their employers conforming that, if granted scholarship will be allowed to utilize these opportunities;
- In order to be nominated, all applicants must submit the filled application forms accompanied with the attached certified photocopies of the academic certificates to the address below before 20th November 2019.
Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
Government City,
Mtumba Block,
Afya Street,
P.O. Box 10,
40479 DODOMA.
Alhamisi, 22 Agosti 2019
BENKI YA DUNIA YAPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUTOA KIPAUMBELE KWENYE SEKTA ELIMU
Benki ya Dunia imepongeza
Serikali ya Tanzania kwa kutoa kipaumbele
kwa sekta ya Elimu na kwamba ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa sana
katika kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanapata nafasi hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa
jijni dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia ukanda wa nchi za
Africa Anne Kabagambe alipofanya ziara katika shule ya Sekondari Kibasila akiwa
na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari
Kibasila ya Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara
katika shule hiyo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya
Afrika Anne Kabagambe.
Mkurugenzi huyo ametembelea
shule ya Kibasila kwa sababu Benki ya Dunia inaendelea kushirikiana na Serikali
ya Tanzania katika juhudi zinazofanywa katika sekta ya elimu ikitambua kuwa
elimu ni ndio chimbuko la maendeleo katika katika nchi yoyote.
Nae Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amesema Benki ya Dunia imekuwa
ikishirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa Elimu unaojulika kama Lipa
Kulingana na Matokeo (EP4R) ambapo Benki ya Dunia imetoa dola za kimarekani
milioni 202 katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2014 na unategemewa
kumalizika mwaka 2021.
Walimu wa shule ya Sekondari
Kibasila iliyopo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati alipotembelea shule hiyo
akiwa na ugeni kutoka Benki ya Dunia.
Waziri Ndalichako amesema
kupitia mradi huo takribani Sh bilioni 141 zimeshatumika kwa ajili ya kukarabati
shule kongwe 62, kujenga vyumba vya madarasa 2,876, matundu ya vyoo 6,558,
nyumba za walimu 59, mabwalo 76, majengo ya utawala 16, Mabweni 533 kwa ajili
ya kuwaepusha watoto wa kike na changamoto za mbalimbali, pamoja na kujenga
mifumo ya maji safi kwenye baadhi ya shule ambazo hazikuwa na vyanzo vya maji.
Aidha Waziri Ndalichako
alisema kwa upande wa Shule ya Sekondari Kibasila shilingi milioni 900 zimetengwa kwenye bajeti
ya mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya
ukarabati na tayari wataalamu wameanza
kufanya tathmini ya majengo ya shule hiyo ambayo ukarabati wake utaanza wakati
wowote kuanzia sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe akizungumza na walimu wa shule ya
sekondari Kibasila wakati alipotembelea shule hiyo. Ameipongeza serikali kwa
kutoa kipaumbele kwenye sekta ya elimu.
Awali akitoa taarifa ya
shule Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila Yasinta Matilya amesema moja ya
changamoto inayokabili shule hiyo ni utoro wa wanafunzi unaotokana na
changamoto za kifamilia ikiwemo watoto kulelewa na mzazi mmoja, kipato duni,
umbali wa makazi ya wanafunzi.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti wanafunzi wa shule hiyo wameiomba Serikali kuwapatia walimu wa
saikolojia watakaowasaidia kujitambua ikiwa ni pamoja na kuwajengea mabweni ili
kuepukana na vishawishi vya barabarani pamoja na usumbufu wa usafiri wa
unaopelekea wanafunzi kuacha shule.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe mara baada ya kuhitimisha
ziara katika shule ya sekondari kibasila iliyoko jijini Dar es Salaam.
Jumatatu, 19 Agosti 2019
WAZIRI NDALICHAKO AWAASA WANAFUNZI WALIOPATA UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU NCHINI CHINA KUWA MABALOZI WAZURI
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewaasa wanafunzi
waliopata ufadhili wa masomo ya Elimu ya juu nchini China kuwa mabalozi wazuri
wa Tanzania nchini humo.
Waziri
Ndalichako amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga
wanafunzi hao iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa China nchini.
Jumla
ya wanafanzi 61 wamepata ufadhili wa masomo kwa Shahada za Uzamili na Uzamivu katika fani za Afya,
Uhandisi, Utabibu , TEHAMA na Mazingira.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiteta jambo na Balozi wa China nchini Wang Ke. |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Balozi wa China nchini Wang Ke zawadi ya picha inayoonesha baadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi za Tanzania. |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China. |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)