Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Mbulu,
mkoani Manyara kuhakikisha inatafuta fedha za kukamilisha miradi ya elimu
inayosimamiwa na Wilaya hiyo katika kipindi cha miezi mitatu.
Ole Nasha ametoa agizo hilo
baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo na kukuta haijakamilika kutokana na
halamashauri hiyo kukosa fedha za kukamilisha hali iliyosababishwa na kutofuata
maelekezo ya mradi huku wakipanga kuchangisha wazazi wa wanafunzi wanaosoma
katika shule hiyo ili kukamilisha miradi hiyo.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua moja ya bweni
linalojengwa na Wizara kupitia fedha za EP4R katika Shule ya Sekondari ya Chief
Sarwatt iliyoko katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu mkoani Manyara
Naibu Waziri ametaja miradi
hiyo kuwa ni pamoja na ule wa ujenzi wa mabweni, madarasa na matundu ya vyoo ndio
ambayo inatekelezwa katika shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo katika kata
ya Endagikot Mkoani humo na kutaka ikamilike bila kuhusisha wanafunzi ama
wazazi wao.
“Suala kuchangisha wanafunzi liko wazi kwa
kila mtu, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
amekataza suala la kuchangisha mwanafunzi au mzazi wa mwanafunzi yeyote eti kwa
kuwa mwanafunzi anasoma katika shule fulani, suala la michango linatakiwa
kuhusisha jamii nzima bila kujali huyu ni mzazi wa mwanafunzi ama la na
linafanyika kupitia ofisi ya Mkurugenzi na si walimu na katika hili mlipaswa
kuishirikisha jamii kabla ya kuanza ujenzi,” alisisitiza Naibu Waziri Ole
Nasha.
Naibu Waziri Ole Nasha
alisema Wizara ya Elimu ilitoa fedha kiasi cha Shilingi milioni 215,500,000 kwa
ajili ya ujenzi wa mabweni 2 ya Wanafunzi, vyumba vitatu vya madarasa na
matundu matano ya vyoo na kupaswa kutekelezwa kulingana na maelekezo, lakini
halmshauri ilikuja na mpango mwingine wenye makisio tofauti na yale ya Wizara.
“kama mliona kuna
chanagamoto mlipaswa kushirikisha Wizara kabla ya kufanya maamuzi mliyofanya
ingesaidia kuondokana na kasoro ambazo zinaonekana sasa, na hiki si kitu kipya
zipo Halmashauri zinapekelewa fedha kwa ajili ya Hosteli lakini wanaiomba
Wizara kubadilishiwa kulingana na uhitaji walionao kwa wakati ule mngefanya
hivyo kabla ya kuanza ujenzi ili kupata maelekezo,” aliongeza Naibu Waziri Ole
Nasha.
Muonekano wa hatua
iliyofikiwa ya ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari ya Chief Sarwatt
iliyoko katika halmashauri ya mji wa Mbulu mkoani Manyara
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya
shule ya Chief Sarwatt Emmanuel Tangao alisema walifikia hatua ya kuanza ujenzi
bila kuwashirikisha wananchi kwa kuwa walikuwa wakikimbizana na tamko la
Serikali kwamba mwaka huu walipaswa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano,
lakini pia watakapoishia wangejua ni kiasi gani cha fedha kilichohitajika kukamilisha
ujenzi ndipo wachangishe.
Naibu Waziri Ole Nasha amekamilisha
ziara yake ya kikazi mkoani Manyara ya kukagua uboreshaji wa miundombinu ya
kujifunzia na kufundishia inayotekelezwa katika Halmashauri za Babati, Hanang,
Mbulu na Mbulu, pia alitembelea na kukagua Shule ya Sekondari Gehandu, Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo wa
kile wanachojifunza kutoka kwa mwanafunzi anayechukua kozi ya huduma za mifugo
katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Tango kilichopo Halmashauri ya mji wa
Mbulu Mkoani Manyara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.