JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA
SHULE
ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU
MWAKA
2015/16
Kumekuwepo na Tangazo la
upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa na
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii.
Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki
nazo.
Aidha, Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi
ya Cheti, Stashahada na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI
baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi
wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na
zoezi hilo.
Kutokana na mgawanyo wa
majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa
mwaka huu wa fedha zitatangazwa na
Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara
watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.
Katibu
Mkuu,
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
23 Machi, 2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.