JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
MAADHIMISHO
YA WIKI YA ELIMU MWAKA 2015
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na
Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
inawatangazia wadau wa Elimu na wananchi wote kwa ujumla kuwa Maadhimisho ya
Wiki ya Elimu kwa mwaka 2015 yatafanyika kuanzia mwezi April 2015 hadi Mei
2015.
Maadhimisho haya yatafanyika kwa mara ya Pili kitaifa mwaka
huu 2015.
Maadhimisho ya Wiki ya Elimu yataanzia katika ngazi za Halmashauri, Mikoa na baadaye kuhitimishwa
kitaifa. Uzinduzi wa maadhimisho hayo kitaifa utafanyika
tarehe 11/05/2015 katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo mgeni Rasmi atakuwa
ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter
Pinda. Kilele cha Maadhimisho kitafanyika tarehe 15/05/2015 katika Uwanja wa Jamhuri
mkoani Dodoma ambapo mgeni Rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pamoja na kuongea na wananchi atatoa
zawadi mbalimbali kwa wanafunzi, shule, mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri
na zilizoongeza ufaulu kwa kiasi cha Juu katika Mitihani ya Taifa Darasa la Saba na Kidato cha Nne mwaka
2014.
Maadhimisho ya kitaifa yataenda sambamba na maonesho ya
wadau mbalimbali wa elimu yatakayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani
Dodoma kuanzia tarehe 11-15/05/2015.
Ili kufanikisha maonesho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi inakaribisha wadau wote wa Elimu na Mafunzo kushiriki katika Maadhimisho
hayo katika ngazi za Halmashauri, Mikoa na Taifa.
.
Elimu
Msingi ni Haki ya Kila Mtoto kwa Maendeleo ya Taifa
IMETOLEWA NA:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
7 Mtaa wa Magogoni,
11479 DAR ES
SALAAM.
Tovuti: www.moe.go.tz
19/04/2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.