Waziri Mkuu alisema hayo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya elimu kitaifa yanayofanyika kwa mara ya pili nchini katika uwanja wa Jamhuri, Mjini Dodoma. Maadhimsho haya yaliyoanza tarehe Mei 11 yanakwenda sambamba na maonesho ya wadau mbalimbali wa Elimu na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Ijuma tarehe Mei 15 na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Aidha, katika ufunguzi huu Mhe. Waziri Mkuu ametoa tuzo kwa Shule, Mikoa na Halmashauri zenye ufaulu uliotukuka na zilizoongeza ufaulu kwa kiwango cha juu katika mitihani 2014 ikilinganisha na matokeo ya 2013. Sambamba na utoaji wa tuzo pia alitoa pikipiki kwa Waratibu Elimu Kata sita waliowakirisha Waratibu Elimu Kata wa nchi nzima
Hayo maadhimisho yalikuwa yakibamba kweli!!
JibuFuta