Wataalam
wa Elimu kutoka Sweden ambao ni Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Juu nchini humo
wameanza ziara ya kikazi nchini kwa
lengo la kujifunza mfumo wa elimu katika ngazi zote, mipango ya maendeleo
pamoja na mageuzi mbalimbali ya Elimu.
Wataalam hao ni Wakaguzi wawili toka Kitengo
cha Elimu ya Juu (Cecilia George na Petra Nord); Wakaguzi wawili kutoka Kitengo
cha Elimu ya Sekondari (Eva Neihoff na Isabelle Nilsson); na Mkaguzi mmoja toka
katika Kitengo cha Elimu ya Ufundi (Stefan Lofkvist).
Ujumbe
huo umekutana na kufanya mazungumzo na watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi wakiongozwa na Kamishna wa
Elimu nchini Prof. Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu Mkuu. Mazungumzo
yao yalijikita zaidi katika kubadilishana uzoefu kuhusu mifumo ya elimu
inayotumika katika nchi hizo mbili.
Aidha,
wataalam hao katika ziara yao iliyoanza tarehe 5 hadi 7 Oktoba, 2015 wanatembelea taasisi zilizo chini ya Wizara
zikiwemo; Taasisi ya Elimu Tanzania, Baraza la Mitihani, Tume ya Vyuo Vikuu, Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi. Pia watatembelea shule mbili za sekondari
zenye kidato cha tano na cha sita kwa lengo la kuanzisha uhusiano wa kirafiki na
shule kama hizo nchini Sweden.