Mkutano wa kutathmini Sekta ya Elimu nchini kwa
mwaka 2015 umefanyika jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia tarehe 28 hadi 30 Septemba, 2015 ambapo
Wadau mbalimbali wa Elimu ikiwa ni pamoja na Serikali, Washirika wa Maendeleo na
Taasisi Zisizokuwa za Serikali zinazojihusisha na Elimu walikutana na
kujadiliana kuhusu mafanikio, changamoto na mikakati ya kuboresha elimu nchini.
Mkutano
huo ambao ulifanyika sambamba na Maonesho ya Matumizi ya TEHAMA katika Elimu ya
Msingi ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Profesa Sifuni Mchome ambae aliwataka washiriki wa mkutano huo kujadili kwa
kina namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika Sekta ya
Elimu nchini.
Mkutano huo umefungwa na Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anaeshughulikia Elimu Mhe.
Kassimu Majaliwa ambae alisema ushirikiano ulioko kati ya Serikali na Washirika
wa Maendeleo unasaidia kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika kuimarisha
mahudhurio ya shule, kugharamia Elimu
Msingi kwa wanafunzi wote,
kupatikana kwa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati katika Elimu Msingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.