WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROFESA JOYCE NDALICHAKO AWAFUKUZA WALIMU 4 WALIOSHIRIKI KUMPIGA MWANAFUNZI MBEYA.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa JOYCE
NDALICHAKO ametangaza kuwafukuza chuo walimu wanafunzi walioshiriki kitendo cha
kumpiga mwanafunzi wa kidato cha TATU katika shule ya kutwa ya Sekondari mkoani
MBEYA.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini DSM waziri
NDALICHAKO amesema kuwa kitendo hicho ni cha kikatili, jinai na kuwa walimu hao
wanafunzi hawafai kuendelea na taaluma hiyo ya ualimu na kuwa hatua zaidi za
kisheria zinaendelea kuchukuliwa.
Waziri NDALICHAKO amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu za
vyuo vikuu kitendo kilichofanyika ni kosa la jinai na kuwa hakiwezi kufumbiwa
macho.
Waziri pia ametoa onyo kali kwa wanafunzi wanaokwenda kwenye
mazoezi kwa vitendo na kuwa kwenda
kinyume na taaluma, mwanafunzi wa vitendo
anakuwa amepoteza sifa hivyo amewataka kuzingatia maadili ya fani
na taaluma wanazozisomea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.