Jumatatu, 17 Oktoba 2016



WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA



TAARIFA KWA UMMA

YAH: UHAKIKI WA VYUO NA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO YA SHAHADA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote  vinavyotoa shahada nchini  vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.

Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada  nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:


Katibu Mkuu

17/10/2016

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.