Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Sylivia Temu amewataka Wazazi, walezi na walimu
kuwalea watoto katika misingi ambayo itawafanya wawe na maadili
mema ili waje kuwa viongozi, na wazazi bora katika maisha yao ya baadae.
Profesa Temu amesema hayo hii leo katika maadhimisho ya kilele
cha siku ya mtotot wa Afrika ambayo yamefanyika kwenye kijiji cha Humekwa,
Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Profesa Temu amesewasihi Watoto kupenda kusoma na kuacha
kujiingiza kwenye makundi ya matumizi ya dawa za kulevya, na badala yake
watoto wajikite zaidi katika kusoma kwa bidii ili wawe viongozi bora na
wenye maadili sahihi katika taifa letu.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ni:
Maendeleo Endelevu 2030 " Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.