Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako
amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi wa wamiliki wa shule
binafsi za sekondari ambapo kwa pamoja
wamejadili utekelezaji Wa waraka Namba. 7 unaokataza wanafunzi kufukuzwa
shule kwa sababu ya kutofikisha wastani wa ufaulu uliowekwa na shule.
Waziri Ndalichako ameeleza ameeleza kuwa
chimbuko la waraka huo ni baadhi ya shule kufukuza idadi kubwa ya wanafunzi
wakiwa Mwaka wa mwisho wa masomo yao kwa kigezo cha kutotimiza wastani
unaotakiwa kitendo ambacho amekielezea kuwa kuwa ni cha kibaguzi na
ki-unyanyasaji.
" Mfano shule ya sekondari Pandahil ambayo imefukuza
watoto 148, shule ya sekondari star high imefukuza wanafunzi 49 hizo ni baadhi
tu, Aidha, ameeleza kuwa Wakati Bunge
na Serikali ikisikitika pale Wasichana wanapopata uja uzito na kuacha shule,
Waja sekondari na Musindi sekondari zimefukuza wanafunzi wa kike 15 kila moja
kwa kigezo cha ufaulu mdogo.
Waziri huyo amesisitiza kuwa
wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa waraka huo na amewataka Viongozi hao
kuweka utaratibu mzuri kwa wanafunzi walio na uwezo mdogo badala ya utaratibu
uliopo sasa wa kuwafukuza shule na hivyo kuwaacha wakiwa hawana pa kwenda.
Kwa upande wao viongozi wa
wamiliki wa shule wameeleza kuwa utekelezaji wa waraka huo utasababisha
kushukuka kwa Ubora Wa ufaulu katika shule zinazomilikiwa na watu binafsi.
Kikao hicho pia
kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo kikao ambacho kimefanyika
jijini Dar es salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.