Waziri wa Elimu, Sayansi na
Tekolojia Profesa Joyce Ndalichako leo
amezindua bodi ya ushauri ya wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)
ambapo ameitaka bodi hiyo iisaidie ADEM
kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa
upande wa kutoa mafunzo, nidhamu ya utendaji kazi na kusimamia vyema matumizi
sahihi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya Taasisi hiyo.
Waziri Ndalichako ameyasema
hayo hii leo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kusisitiza kuwa anategemea kuona
matokeo chanya kutoka kwenye bodi hiyo kwa kuwa wote walioteuliwa wamebobea
katika masuala mbalimbali yanayohusu Elimu.
Akizungumza mara baada ya maelekezo
ya Waziri Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Naomi Katunzi amemhakikishia Waziri
Ndalichako kuwa bodi hiyo itafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.
Dk. Katunzi amesema kuwa
wamepokea kwa mikono miwili uteuzi huo na kuwa watahakikisha wanafanya kazi kwa
ushirikiano wa hali ya juu Kati ya bodi na uongozi wa ADEM.
Kwa upande wake Mtendaji
Mkuu wa wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu
Dk. Joseph Masanja amesema bodi
hiyo itaishauri ADEM katika masuala mbalimbali ili kufikia malengo
yanayokusudiwa.
Bodi hiyo ambayo
imezinduliwa leo itatekeleza majukumu yake katika kipindi cha miaka Mitatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.