Serikali
ya awamu ya Tano imesema katika kulinda
haki za mtoto imedhamiria kujenga shule za Elimu Jumuishi na zile za wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika kila
mkoa.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave maria Semakafu jijini Dar es Salaam wakati
akifungua mkutano wa kimataifa wa wadau unaojadili haki za mtoto.
Naibu Katibu Mkuu Dk. Ave maria Semakafu
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu haki za mtoto,
mkutano ambao umefanyika jijini Dar es salaam.
Dk.
Semakafu amesema lengo la ujenzi wa shule hizo ni kuhakikisha watoto wote wa
kitanzania wapata Elimu bila vikwazo vya aina yoyote kwani Elimu ni msingi wa
Maenedeleo.
Amesema
katika kutekeleza hilo tayari Wizara hiyo inajenga shule ya mfano kwa ajili ya
wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika chuo cha Ualimu Patandi kilichopo
mkoani Arusha, ambapo shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wa
shule ya msingi mpaka Sekondari.
Wageni waalikwa katika meza kuu
wakifuatilia majadiliano kupitia jukwaa la kutetea haki za mtoto.
Naibu
Katibu Mkuu huyo amewataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wote wenye
umri wa kwenda shule bila kuangalia changamoto za kimaumbele walizonazo watoto
wao kwa kuwa tayari Serikali imewekeza katika eneo hilo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano unaojadili
haki za mtoto wakisikiliza kwa makani hotuba ya Naibu katibu Mkuu Dk. Semakafu
(hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa UNICEF katika masuala ya Elimu nchini Tanzania Cecilia Baldeh amesema tayari
Tanzania imekwisha piga hatua katika kulinda na kutetea haki za mtoto ikiwa ni
pamoja na Serikali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule
wanakwenda kwa kuwa Elimu msingi hivi sasa inatolewa bure.
Wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Kimatifa la nchini Sweden, SIDA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Dk. Avemaria
Semakafu kabla ya kufungua mkutano wa wadau wa ndani na nje ya nchi unaojadili
haki za mtoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.