Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce
Ndalichako amesema Serikali itatumia mbinu zote za ufundishaji ili kuwezesha
watoto kujifunza kwa ufanisi.
Waziri Ndalichako amesema hayo jijini Dar es Salaam
wakati wa uzinduzi wa ufundishaji wa maudhui yaliyoandaliwa kwa mfumo wa
kietroniki ambayo yatatumia Vikaragosi (Cartoon) kufundishia watoto wa madarasa
ya chini.
Waziri Ndalichako
amesema njia hii Itasaidia watoto kuelewa kwa
urahisi kwani wapo watoto
wanaoelewa kwa kuona, kushika na kisikiliza.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako akizungumza na Wadau wa Elimu ( Hawapo Pichani) wakati wa uzinduzi wa ufundishaji wa maudhui yaliyoandaliwa
kwa mfumo wa kietroniki ambayo yatatumia Vikaragosi (Cartoon)
"ikumbukwe kwamba hakuna njia bora kuliko nyingine
katika kufundisha, wapo watoto
wanaoelewa zaidi kwa kuona, kusilikiza ama Kufanya kwa vitendo hivyo ni
muhimu kutumia njia zote ili tusiache mtoto yeyote bila kuelewa"
Amesisitiza Waziri Ndalichako
Waziri Ndalichako amesema matumizi ya Vikaragosi yataleta
ari kwa watoto kujifunza kwani wakati wa majaribio ya vikaragosi hivyo
walionyesha hali ya kutaka kujifunza kwa kutumia.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako akionyesha DVD zenye maudhui ya Kietroniki ambazo zitatumika
kufandishia madarasa ya chini wakati wa uzinduzi wa ufundishaji wa maudhui yaliyoandaliwa
kwa mfumo wa kietroniki ambayo yatatumia Vikaragosi (Cartoon)
Aidha, Waziri wa Elimu amewataka Maafisa Elimu Kata kote
nchini kuhakikisha wanafatilia kwa ukaribu ufundishaji kwa kutumia Vikaragosi
hivyo pindi vitakaposambazwa shuleni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.