Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia DK
Leonard Akwilapo amewataka Waandishi wa habari nchini kujikita katika kuandika
habari za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kuleta matokeo chanya katika
kuelekea uchumi wa viwanda.
Akizungumza wakati wa kutoa tuzo za umahiri kwa waandishi
wa habari wa masuala ya Sayansi na Teknolojia zilizoandaliwa na Tume ya Taifa
ya Sayansi na Teknolojia kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Kilimo jijini Dar es
Salaam amesema kuwa Dunia inategemea Sayansi na Teknolojia katika kuleta mabadiliko endelevu ya kimaendeleo
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akimkabidhi mmoja wa washindi wa tuzo za
umahiri kwa waandishi wa habari ya Sayansi na Teknolojia zilizoandaliwa na Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Kilimo zilizofanyika
jijini Dar es Salaam
Aidha, ameipongeza
tume hiyo kwa kuona umuhimu wa kutoa taarifa ya nini inafanya kwa wananchi kwa
kuwahusisha waandishi wa habari ambao wamekuwa wakitoa taarifa hizo kwa jamii
kupitia vyombo vya habari
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia Dk. Amos Nungu amesema tuzo hizo zimeshirikisha kazi 56
kutoka katika vyombo 10 vya habari na kutoa wito kwa Waandishi wa Habari kujitokeza
kwa wingi kushiriki katika kuelimisha jamii mambo mbalimbali yanayohusu Sayansi
na Teknolojia.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo
akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wanasayansi (hawapo
pichani) wakati wa kutoa tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa Sayansi na
Teknolojia ambapo amewataka waandishi wa habari kujikita katika kuandika
masuala ya sayansi na teknolojia ili kuwezesha wananchi kufikia uchumi wa
viwanda wakiwa na taarifa sahihi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.