Jumatano, 10 Oktoba 2018

WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA WATANZANIA KUUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA RAIS MAGUFULI

 Watanzania wametakiwa kushikamana kwa kufanya Kazi kwa bidii kwa lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na  Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt. John Magufuli ili Taifa liweze kutumiza malengo ya  kufikia uchumi wa kati hadi ifikapo  mwaka 2025.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya 19 ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere linalofanyika katika chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka watanzania kuunga mkono kwa vitendo juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli ili Taifa liweze kufikia mafanikio yake.

Waziri Ndalichako amesema Wizara itaendelea kukienzi Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kiendelee kuwa  Kitovu cha maadili katika kuwajenga Viongozi na vijana ikiwa ni pamoja  na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho  Prof. Shadrack Mwakalila amewataka viongozi na wanafunzi kuhakikisha wanakitumia chuo hicho kwa ufanisi ili kupata  mafunzo  yanayohusu uzalendo, uadiifu na kuwa mafunzo yanayotolewa  chuoni hapo ni yale ya muda mfupi na mrefu.  

Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara hiyo Moshi Kabengwe, na Mkuu wa chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila.

Prof. Mwakalila amesema kila mwaka chuo hicho huandaa maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati wa Baba wa Taifa kwa Lengo la kujitathmini kama Taifa, tumetoka wapi na tuko wapi.

Katika kumbukizi hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa  ikiwemo ile inayohusu Uhuru na Maendeleo katika kuelekea uchumi wa Kati, umuhimu wa uzalendo na uadilifu, umuhimu wa misingi ya Azimio la Arusha katika kustawisha Viwanda vya ndani.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mkurugenzi anaesimamia idara ya Ufundi katika Wizar hiyo Dkt. Noel Mbonde.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.