Naibu waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Willam Ole Nasha amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Mbulu
Chelestine Mofuga kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika
kubadilisha matumizi ya fedha za miradi ya Shule ya Sekondari Tumatu iliyoko
Wilayani Mbulu Mkoni Manyara.
Mheshimiwa Ole Nasha ametoa
agizo hilo wakati akikagua ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Elimu mkoani
humo na kukuta fedha zilizotolewa na Wizara ya Elimu kiasi cha sh milioni 141,
600,000 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya ya madarasa, bweni na vyoo
zimetumika kukamilisha jengo la bweni na maktaba ambavyo vilijengwa kwa nguvu
za wananchi.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua ujenzi wa
bweni katika Shule ya Sekondari Tumatu wilayani Mbulu Mkoani Manyara
Naibu Waziri Ole Nasha
amesema shule hiyo ilipatiwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa bweni
moja la wanafunzi, madarasa 3 na matundu ya vyoo 6 lakini fedha hizo
hazikuelekezwa kwenye kile kilichokusudiwa badala yake zimetumika kukamilisha
majengo ambayo tayari wananchi walianza kujenga kwa gharama ambazo hazina
uhalisia.
"Hapa kuna harufu ya ubadhirifu wa fedha
za umma haiwezekani gharama za kumalizia majengo ambayo tayari wananchi
wameanza kujenga na kukaribia kukamilika kutumia fedha za kujenga majengo
mapya, kujua hili haiitaji mtu kuwa mhandisi ni mahesabu ya kawaida tu, hatua
zichukuliwe dhidi ya waliohusika.” Aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa maelekezo kwa
Viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Mbulu kuhusu ujenzi wa bweni la
Wasichana uliofanyika katika Shule ya
Sekondari Tumatu iliyoko katika Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.
Naibu Waziri Ole Nasha
amesema Serikali ya Awamu ya Tano ya
Mhe. Dk. John Pombe Magufuli inatoa kipaumbaele kwenye Sekta ya Elimu na ndio
maana kila mahali kuna miradi ya Elimu hivyo fedha za miradi zitumike vizuri na
kwamba haitasita kuchukua hatua dhidi ya mtu yeyote atakaebanika anafanya
ubadhirifu wa fedha za miradi hiyo.
Kufuatia agizo hilo Mkuu wa
Wilaya hiyo amewaweka chini ya ulinzi kwa saa 48 wafanyakazi hao ambao ni Afisa
Elimu Sekondari wa Wilaya ya Mbulu Ludovic Longino, Fundi Sanifu (Civil
tehnician) wa Halmashauri Moses Nguvava, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Bryson
Panga, Mkuu wa shule hiyo Killian John na Afisa Ugavi Faustine Safari kutokana
na tuhuma hizo na kuagiza TAKUKURU kuanza uchunguzi mara moja.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongea na wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Yaeda Ampa pamoja na wanakijiji wa eneo hilo ambapo
kwa pamoja amewataka kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano
anazozifanya katika kuboresha Sekta ya Elimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.