Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo amezindua mwongozo
na mashindano ya ubunifu kitaifa mkoani Dodoma.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi Waziri Ndalichako amesema lengo la mashindano
hayo ni kutambua na kuendeleza fikra za wabunifu kwa lengo la kuongeza ajira.
Prof.
Ndalichako amesema katika kuimarisha uchumi wa viwanda lazima matumizi ya
Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaimarishwe kwa lengo la kuongeza tija viwandani
na kwenye biashara.
“Kutoka
na umuhimu wa mashindano haya naielekeza Idara ya Sayansi, Teknolojia na
ubunifu kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kila mwaka, ili kukuza ujuzi,
wabunifu kwa maendeleo ya viwanda,” alisisitiza Waziri Ndalichako.
Waziri
Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba
wakionesho mwongozo wa Ubunifu mara baada ya Kuzinduliwa leo Jijini Dodoma.
Mashindano
hayo yameshirikisha Makundi mbalimbali ya kijamii zikiwemo Shule za Sekondari,
Vyuo vya Ufundi Stadi, Sekta isiyo rasmi, Vyuo vya ufundi wa Kati, Vyuo vya
Elimu ya Juu na Taasisi za utafiti na Maendeleo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya
Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa kuzinduliwa kwa mwongozo huo ni jambo
kubwa na la kihistoria ikizingatiwa kuwa nchi inaelekea kwenye uchumi wa
viwanda.
Serukamba
amesema bila Sayansi, Teknolojia na ubunifu nchi haiwezi kufanikisha
malengo yake, hivyo ameiomba Serikali ihakikishe inawekeza fedha nyingi.
“Kama
hatutawekeza fedha za kutosha kwenye Sayansi, Teknolojia na Ubunifu hatuwezi
kufanya kitu, hivyo tuwekeze fedha za kutosha ili tujiletee Maendeleo kwa
haraka,” amesema Mhe. Serukamba.
Kauli
mbiu ya mashindano hayo ni “Kukuza Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda.”
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi mmoja wa
Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Dodoma Mwongozo wa Ubunifu mara baada ya
kuuzindua leo Jijini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.