Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka walimu nchini kote kuachana
na aina ya zamani ya ufundishaji na badala yake watumie mbinu za kisasa ili
kusaidia kumuandaa mwanafunzi aweze kuendana na mabadiliko ya Sayansi na
Teknolojia.
Mheshimiwa Ole Nasha
ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya
Elimu na kuongea na Viongozi wa Elimu ngazi ya Mkoa ambapo amesisitiza kuwa Elimu ya sasa ni ile ambayo inaendeshwa na matumizi ya Tehama, uongozi mzuri na
kubadili mtizamo wa Elimu kutoka katika utaratibu ule ambao mwanafunzi anakuwa
mtu wa kupokea na kwenda kwenye mfumo ambapo mwanafunzi anategemewa kushiriki zoezi la ufundishaji.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua samani katika
Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyojengwa Wamo Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri huyo pia amesema katika vyuo mfumo unaotumika ni ule wa kumuandaa
mwanafunzi kwenda kuajiriwa badala ya kujiajiri mwenyewe hali ambayo inabidi
kubadilika ili vijana waweze kumaliza wakiwa wenye maarifa ya kwenda kutatua
changamoto zilizopo katika jamii.
“Katika vyuo vyetu, mfumo wa sasa unaotumika unawafundisha wanafunzi
kama watu wa kwenda kufanya kazi baadae badala ya kufundisha watu wa kwenda
kutengeneza ajira na ndio maana mwanafunzi akimaliza chuo anakuja ofisini
anasubiri umpe kazi, hiyo siyo sawa lazima Elimu yetu iwe ni ya kujenga maarifa
ya kujitegemea“ alisisitiza Mhe. Ole Nasha
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na wanafunzi
wanaosoma katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima iliyoko Wamo mjini Morogoro.
Naibu Waziri Ole Nasha pia amewataka
viongozi wa mkoa wa Morogoro kufuatilia kwa karibu miradi ya Elimu inayotekelezwa
katika mkoa huo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango
vinavyokubalika.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Joyce Balavuga alimweleza
Naibu Waziri wa Elimu kuwa mkoa wa Morogoro uko mstari wa mbele kuhamasisha matumizi
ya Tehama katika ujifunzaji na ufundishaji katika shule zake ili kuinua kiwango
cha ufaulu, kutunza kumbukumbu na takwimu mbalimbali za Elimu.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji William Ole Nasha akikagua mradi wa
ujenzi wa karakana za ufundi umeme zilizojengwa katika Chuo cha Ufundi na
Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Kihonda mjini Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.