Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) kuchunguza mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya ujenzi wa Mradi wa
Chuo Cha Ufundi stadi VETA mkoani Geita unaotekelezwa na Kampuni ya ukandarasi
inayojulikama kama SkyWard.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua mradi wa ujenzi
wa Chuo cha Ufundi Stadi, VETA mkoani Geita wakati wa ziara yake ya mkoani
humo.
Waziri huyo amesema
hajaridhishwa na ujenzi wa mradi huo na kuwa hadi sasa tayari ni miezi
mitano na kwa mujibu wa mkataba bado miezi
sita mradi ukabidhiwe, lakini inavyoonekana ni kuwa kampuni hiyo tayari
ilishaonesha kushindwa kazi ambayo walishapewa ya ujenzi wa Chuo Cha Ualimu
Ndala.
“Mkandarasi hii Serikali
siyo ya kuichezea, mwaka mzima sasa bado mko asilimia ambazo haziridhishi pia
hakuna kasi ya majengo na hakuna vibarua wanaoendelea na kazi, mnadeni Chuo cha
ualimu Ndala, na hapa tena kwenye ujenzi
wa Chuo cha VETA Geita kuna tatizo na hata mazingira ya kumpa huyu mkandarasi
kazi, niwaonye watu wa Idara ya manunuzi pale Wizarani kuacha kutoa kazi kwa
watu wasiokuwa na uwezo,” anasema Waziri Ndalichako,
Muonekano
wa moja ya jengo katika mradi wa ujezni wa chuo cha Ufundi Stadi Mkoani Geita,
ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amemtaka
mkandarasi kukamilisha ujenzi huo katika muda uliopangwa na si vinginevyo.
Waziri huyo yuko mkoani
Geita kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa vyuo vya Ufundi stadi
vya Geita na Chato.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa
mkoa wa Geita wakati wa ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi
Stadi kinachojengwa mkoani humo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.