Serikali imekamilisha miundombinu
yote muhimu ikiwemo Maji, umeme na barabara kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa
Chuo cha Ufundi stadi VETA mkoani Kagera.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa
na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako baada ya
kuzindua chanzo cha Maji ambacho kitatumika kwa ajili ya kujenga VETA hiyo
katika kijiji cha Burugo, Kwenye halmashauri ya Bukoba.
“Dhamira ya Serikali ya awamu ya
Tano ni kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo mwaka 2025 ili kutimiza
malengo hayo ndiyo serikali imewekeza zaidi katika kujenga vyuo vya Ufundi
stadi ili kuwa na wataalamu wa kati na wa kutosha watakaotumika kwenye viwanda
hapa nchini,” alisisitiza Waziri Ndalichako.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizindua chanzo cha
maji kitakachotumika kujenga chuo cha Ufundi stadi, VETA mkoani Kagera na kuwa
ujenzi huo unatarajiwa kuanza muda wowote baada ya serikali kukamilisha
miundombinu inaayohitajika kama vile maji, umeme na barabarana.
Awali akipokea taarifa ya mkoa
huo kuhusu sekta ya Elimu, Waziri Ndalichako ameonesha kutoridhishwa na hatua
za ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi mkoani humo na kuzitaka
mamlaka husika kutafuta ufumbuzi ili kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi.
Waziri Ndalichako pia ametembelea na kukagua ujenzi unaoendelea wa Chuo cha Ufundi Stadi Karagwe ambapo amemtaka Mkandarasi kuhakikisha kazi hiyo inakamilika katika muda uliopangwa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua mradi wa ujenzi
wa chuo cha Ufundi stadi VETA, (KDVTC) Wilayani Karagwe mkoani Kagera ambapo
waziri amemuelekeza mkandarasi kukamilisha ujenzi katika muda uliopangwa.
Waziri Ndalichako pia alitembelea Shule ya Bukoba Sekondari ambayo paa za shule
hiyo ziliezuliwa kufuatia mvua kubwa Iliyoambatana na upepo na hivyo kulazimika
wnafunzi wa shule hiyo kuhamishiwa katika shule ya sekondari Ihungo na wengine
katika shule ya Sekondari Omumwani.
Wakala
wa majengo ambaye ndiyo Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi
Karagwe, Kilichopo Wilayani Karagwe akijadiliana
Jambo na Waziri Ndalichako wakati Waziri akikagua ujenzi wa chuo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.