Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka
Wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuacha kulalamika kuhusu
miundombinu ya shule wakati wanashindwa kutumia vyema fedha zinazotolewa na
serikali kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu.
Waziri Ndalichako ametoa
kauli hiyo wakati akifungua mafunzo elekezi kuhusu utekelezaji wa Programu ya
lipa kukingana na Matokeo katika sekta ya Elimu ambapo amewataka watendaji wa
halmashauri kuacha kufanya matumizi tofauti na maelekezo yanayotolewa na kama
upo ulazima wa kubadili matumizi halmashauri zinapaswa kuomba kibali cha
kubadili matumizi na hawatatakiwa kuanza matumizi kabla ya idhini kutolewa.
“Mpango huu wa lipa
kulingana na Matokeo unekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi Cha kuanzia
mwaka 2014/2015 hadi 2017/2018 halmashauri zimekuwa zikifanya vizuri katika utekelezaji wa vigezo
na hivyo kupata ongezeko la fedha kila mwaka kutoka Shilingi bilioni 15.53
(2014/2015) hadi kufikia shilingi bilioni 50 kwa mwaka ( 207/1018),”alisema
Waziri Ndalichako.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na
Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu wa mikoa, maafisa Elimu msingi na
Sekondari na Wathibiti Ubora wa Shule
(hawapo pichani),wakati akifungua mafunzo elekezi kuhusu utekelezaji wa Program
ya Lipa Kulingana na Matokeo katika sekta ya Elimu. Mkutano huo umehusisha watendaji
wa mkoa wa Mwanza na Shinyanga.
Pia Waziri Ndalichako
amewataka Wakurugenzi, Maafisa Elimu na Wathibiti ubora wa shule kuimarisha
mfumo wa menejimenti na upatikanaji wa taarifa /Takwimu za Elimu na kuhakikisha
kunakuwa na usawazishaji wa ikama ya walimu ndani ya halmashauri.
Watendaji
katika sekta ya Elimu wa mkoa wa Mwanza na Shinyanga wakifuatilia hotuba ya Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati akifungua mafunzo
elekezi kuhusu utekelezaji wa Program ya
Lipa Kulingana na Matokeo katika sekta ya Elimu. Amewataka watendaji hao
kufanya kazi zao kwa mipango na weledi.
Lengo la programu ya lipa
kulingana na matokeo ni kuinua ubora wa Elimu nchini na kuwa fedha kupitia
programu hii hutolewa kutokana na kukidhi vigezo vilivyokubalika na kufanyiwa
uhakiki ili kuthibitisha kuwa vimetekelezwa.
Mafunzo hayo ya siku mbili
yamefanyija katika mikoa yote hapa nchini.
Mratibu
wa Mafunzo Elekezi ya EP4R, Lawarence Sanga akitoa maelezo kwa Waziri
Ndalichako kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo kwa watendaji katika kusimamia vyema
fedha za miradi inayotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.