Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amewataka watumishi kufanya kazi
kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za kazi pamoja na kujiepusha na
vitendo vya rushwa.
Dkt. Akwilapo ameyasema hayo
Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja na watumishi wa Wizara hiyo wenye
lengo la kupitia utendaji kazi wa wizara kwa mwaka 2018 na kuweka malengo ya
utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2019.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo
akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), wakati akifungua mkutano
wa pamoja uliofanyika Jijini Dodoma leo, ambao amewataka watumishi kufuata
kanuni, taratibu na sheria za kazi pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoka
Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Dkt. Leonard
Akwilapo wakati wa mkutano wa pamoja wa Watumishi wa Wizara hiyo, mkutano huo
umefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu huyo pia amewataka
watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kuwahudumia wateja kwa lugha nzuri na
kuhakikisha huduma zinatolewa katika muda muafaka kwa lengo la kuepusha
malalamiko.
“Nichukue fursa hii kupitia
mkutano wa wafanyakazi wote kuwataka kutekeleza majukumu yenu kwa kufuata taratibu
na sheria za kazi pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili nchi iweze
kufikia malengo ambayo imejiwekea. Kila mmoja atomize wajibu wake katika eneo
lake naamini kwa kufanya hivyo tutafanikiwa,” alisisitiza Dkt. Akwilapo.
Watumishi
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Makao Makuu) wakiwa katika Mkutano wa
pamoja ambapo Katibu Mkuu ameelekeza watumishi kuhakikisha wanatoa huduma bora
kwa wateja na zitolewe katika muda muafaka.
Mkutano wa pamoja wa Wafanyakazi wa Wizara hiyo hufanyika
kila mwaka kwa lengo la kujitathmini katika utekelezaji wa majukumu ambayo
Wizara inakuwa imejiwekea.
Mkutano
wa pamoja wa Viongozi na watumishi wa Wizara wenye lengo la kupitia utendaji
kazi wa Wizara kwa mwaka 2018 na kuweka malengo ya utekelezaji kwa mwaka 2019.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.