Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako
amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo kuwasimamisha kazi
watumishi 6 wa Chuo cha Ualimu Patandi kutokana na kushindwa kusimamia vyema
ujenzi wa shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu inayojengwa Wilayani
Arumeru mkoani ARUSHA.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akiwa na Mkuu wa Wilaya
ya Arumeru Jerry Muro, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ave Maria Semakafu
na watendaji wengine wakikagua hali ya ujenzi wa shule ya wanafunzi wenye
mahitaji maalumu inayojengwa katika Chuo Cha Ualimu Patandi mkoani ARUSHA.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo baada ya kukagua hali ya ujenzi
unaoendelea wa vyumba vya madarasa, jengo la Utawala, na bwalo la chakula na
kisha kuwa na kikao cha pamoja na watendaji wa Chuo hicho kwa ajili ya kupata
ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo yameripotiwa na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa
Wizara hiyo baada ya kufanyika ukaguzi wa mradi huo wa ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akimuonesha Waziri wa
Elimu Prof. Ndalichako hatua za ujenzi wa shule ya wanafunzi wenye mahitaji
Maalumu inayojengwa Patandi, shule hiyo ikikamilika itakuwa na uwezo wa
kuchukua wanafunzi 640.
Kufuatia hali hiyo, Waziri aliagiza kusimamiashwa kazi kwa
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Issac Myovela, Afisa manunuzi Charles Njarabi,
Mhasibu Rose Kijaka, M/Kiti wa kamati ya mapokezi Peter Mosha na
Msimamizi wa ujenzi huo Israel Mayage.
Wengine ni aliyekuwa Afisa manunuzi wa Chuo hicho Henry Matei
ambaye alihamishiwa Chuo cha Ualimu Monduli na kuwa Waziri ameelekeza arudishwe
chuoni hapo na asimamishwe kazi mara moja.
Muonekano wa Jengo la Utawala la Shule ya
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu inayojengwa katika Chuo cha Ualimu Patandi.
Pia Waziri amemuagiza Katibu Mkuu Dkt. Akwilapo kumpunguzia
majukumu ya kazi Mkuu wa Chuo cha Patandi Lyana Mbaji kutokana na kuwa ni mgonjwa
na badala yake ateuliwe Mkuu mwingine aweze kuendelea na majukumu katika Chuo
hicho.
Mpaka sasa tayari Wizara imekwishatoa kiasi cha shilingi Bilioni
2.3, mradi utakapokamika kiasi ha sh. 2.56 zitakuwa zimetumika.
Muonekano wa Bwalo la Wanafunzi wenye mahitaji
maalumu linalojengwa katika Shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika
Chuo cha Ualimu Patandi, Arumeru mkoani Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.