Jumatano, 27 Februari 2019

WAZIRI NDALICHAKO ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI OFISI ZA WIZARA YA ELIMU KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa ofisi mpya za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zinazojengwa kwenye Mji wa serikali Ihumwa, mkoani Dodoma na kusema kuwa ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua ujenzi wa ofisi za wizara anayoiongoza zinazojengwa katika mji wa serikali uliopo eneo la Ihumwa jijini Dodoma.

Waziri Ndalichako amesema kukamilika kwa ofisi hizo utasaidia utendaji kazi kuimarika kwa kuwa mazingira ya kufanyia kazi yanakuwa ni mazuri zaidi.

“Ofisi kwa ujumla ni nzuri zimejengwa vizuri naamini hata watumishi watakuwa na ari ya kufanya kazi kwa kuwa mazingira yatakuwa bora zaidi.” alisema  Waziri Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi za wizara kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi, Kamishna Msaidizi Aron Lunyungu kutoka Shirika la Magereza.

Waziri Ndalichako pia  amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo kuhakikisha anasimamia kwa ukaribu ujenzi wa jengo pacha la wizara ili liweze kukamilika kwa wakati.

Naye Msimamizi wa ujenzi huo Kamishna Msaidizi Aron Lunyungu kutoka Shirika la Magereza amesema ujenzi umefikia katika hatua ya ukamilishaji na kwamba wanatarajia kukabidhi Jengo la Wizara baada ya wiki mbili kuanzi leo.

Ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia katika mji mpya wa serikali ulianza Desemba 10, 2018.
 
Muonekano wa hatua ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zinazojengwa katika mji wa Serikali uliopo eneo la Ihumwa jijini Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.