Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati akifungua kikao kazi kinacholenga kuwakumbusha wathibiti ubora wa shule wajibu wa utekelezaji wa majukumu yao.
Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Wathibiti Ubora wa Shule wakati akifungua kikao kazi hicho mkoani Morogoro
Waziri Ndalichako pia amesema katika kuboresha mazingira Wizara imejipanga kujenga ofisi 100 za wathibiti ubora wa shule, na kuwa fedha kwa ajili ya shughuli hiyo zipo tayari.
Wathibiti Ubora wa Shule wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wakati wa ufunguzi kikao kazi Cha siku nne kinachofanyikia mkoani Morogoro.
“Wathibiti ubora wa shule ni wadau muhimu kwa Maendeleo ya elimu ya nchi yetu, na kuwa nyingi ndiyo jicho la Serikali na ndiyo maana serikali imeendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi ili kuleta ufanisi,” alisema Waziri Ndalichako.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya uthibiti ubora wa shule Euphrasia Buchuma amesema kikao kazi hicho cha siku nne, kina lenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Idara hiyo, kubadilishana uzoefu miongoni mwao, pamoja na kukumbushana matumizi sahihi ya fedha za Umma.
Wathibiti Wakuu Ubora wa Shule Wa Kanda na Wilaya wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao kazi cha kukumbusha wajibu wa utekelezaji wa majukumu.
Kikao kazi hicho kimeshirikisha wathibiti wakuu ubora wa shule wa kanda na Wilaya zote 11.
Viongozi na baadhi ya ya
Wathibiti Wakuu Ubora Wa Shule wakiwa katika picha ya pamoja .
Hongera waziri kwa kuiboresha Idara
JibuFuta