Serikali imewataka wabunifu nchini kujikita katika kuangalia shughuli za ambazo zinafanyika
katika mazingira yao na wabuni jinsi ya kuzirahisisha kwa kutumia Sayansi na kiteknolojia
ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Ilboru Maximillian Masesa akitoa maelezo kwa Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako juu ya kifaa cha kubaini wanafunzi ambao
wanatumia simu shuleni alichobuni.
Kauli hiyo ya serikali
imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
katika kilele cha Mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu mjini
Dodoma. Waziri Ndalichako pia aliongeza
kuwa eneo la Sayansi na Teknolojia ni muhimu kwa taifa na likitumika vyema
litasaidia kuongeza uzalishaji na
Kurahisisha utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.
“Kwa muda mrefu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikisimamia zaidi Elimu kuliko masuala ya
Sayansi na ubunifu hivyo ni vyema wabunifu waendelee kujitokeza zaidi na wajikitike katika ikubuni mbinu za kurahisisha mifumo ya
shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo
Kilimo, ufugaji na njia bora za upatikanaji wa maji”, alisema Waziri
Ndalichako.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalia ubunifu wa injini
ya Ndege uliofanywa na Emmanuel Chibula kutoka
Musoma, Mkoani Mara wakati wa kilele cha mashindano ya kitaifa ya sayansi,
teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Kwa upande wake Kaimu Katibu
Mkuu Profesa James Mdoe amesema
lengo la Mashindano hayo
yaliyohusisha wabunifu kutoka ngazi
mbali za Elimu ni kuibua ubunifu, umahiri, kuchochea ugunduzi kwa lengo la
kukuza matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika maendeleo.
Wanafunzi
mbalimbali wa Shule za Msingi na baadhi ya Wananchi wakifuatilia Mashindano ya
Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere.
Mashindano hayo yalifunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mhe.
William Ole Nasha Machi 5, 2019 na leo yamefikia kilele ambapo washindi
mbalimbali walipata zawadi za fedha na kutunukiwa vyeti.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na washiriki
mbalimbali hawapo pichani wakati wa kufunga mashindano ya kitaifa ya kitaifa ya
sayansi, teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Kauli mbiu ya mashindano
hayo kwa mwaka huu ni " kukuza ujuzi na ubunifu kwa uchumi wa
viwanda".
Wanafunzi wa Chuo cha
Usafirishaji nchini NIT wabuni gari lisilotumia injini, na badala yake
linatumia umeme kuendesha mifumo yake. Pichani Waziri akiwa kwenye gari hilo
akipewa maelezo ya namna gari hilo linavyofanya kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.