Jumamosi, 13 Aprili 2019

SERIKALI KUJENGA SEKONDARI NA CHUO CHA UFUNDI DODOMA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kujenga shule ya Sekondari  na  Chuo cha Ufundi katika jiji la Dodoma ili kutoa fursa za elimu kwa wakazi wa jiji hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mji wa kiserikali jijini Dodoma Rais wa Jamhuri wa Muungano  wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli amesema shule hiyo ya sekondari itakayojengwa kwa Sh. Bilioni 13 itachukua wanafunzi wa  kidato cha kwanza hadi cha sita.
 
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa Serikali, wananchi pamoja na watumishi wa serikali wakati wa uzinduzi wa Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma.
Rais Magufuli ameongezea kuwa  Sh Bilioni 18 pia zitatumika kujenga Chuo kipya kikubwa cha ufundi kitakachotoa mafunzo ya ufundi wa aina mbalimbali jijini Dodoma.

Rais Magufuli amewataka wananchi wa Dodoma kuhakikisha wanatumia vyema taasisi hizo za elimu katika kuwapatia maarifa vijana wao kwa maendeleo ya Dodoma na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waliofika Jijini Dodoma kuhdhuria uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba ambapo Ofisi za Serikali zimejengwa.
Rais Magufuli amezindua mji wa kiserikali katika eneo la Mtumba jijini Dodoma ambapo majengo hayo yatatumiwa  Wizara mbalimbali na baadhi ya Taasisi.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara Mbalimbali  wakati wa uzinduzi wa Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Wizara Mbalimbali  wakati wa uzinduzi wa Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni