Ijumaa, 26 Julai 2019

TAARIFA KWA UMMA


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY


PARTIAL SCHOLARSHIPS TENABLE IN MOROCCO FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020
Call for Application
The General Public is hereby informed that the Kingdom of Morocco through the Moroccan Agency of International Cooperation (AMCI), has granted a scholarship programme to eligible Tanzanian Nationals to pursue  Undergraduate and Postgraduate  studies  at Moroccan Public Institutions for the academic year 2019/2020.
A directory of Training Institution is available on the website of AMCI through  www.amci.ma containing a complete list of the Moroccan Public Institutions of Higher Education as well as specific information about them, including the conditions of access, the subjects and the duration of the studies.
General Admission Requirements  
(i)        Undergraduate Studies
(a)   Bachelor Degree
1.      Applicant must have completed Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSE) in 2018-2019 and pass with Division I or II / Diploma with minimum of Upper Second Class;
2.      Age not older than 23 years by August 2019;
3.      Not  admitted in any Higher Learning Institution in the country; and
4.   Medical Certificate issued by public medical hospitals certifying that
     your are not suffering from any contagious illness or carrying a   
     pandemic.

(ii)              Postgraduate
(a)   Masters:
1.      Must be holders of a first degree with a minimum of Upper Second Class;
2.      Not admitted in any Higher Learning Institution; and
3.      Medical Certificate issued by public medical hospitals certifying that
      your are not suffering from any contagious illness or carrying a   
      pandemic.

(b)  PhD
            1.      Must be holders of Master’s degree in the required subject/specialties   
                        of studies recognized as being equivalent to Moroccan granted    
                        certificate;
           2.      Not admitted in any Higher Learning Institution;
           3.      Medical Certificate issued by public medical hospitals certifying that
      your are not suffering from any contagious illness or carrying a   
      pandemic.

NB:
·         Applicants with a certificate  level of training  in French language will have            an added advantage;
·         For all programmes  the language of instruction is French except for Islamic           and Arabic Literature which will be conducted in Arabic Language;
·         Application forms can be downloaded at: http://www.amci.ma/fcf.pdf
·         There is no Loan or grant  from the Goverment of Tanzania  for candidates          who will be offered this Scholarship.

       List of documents to be submitted include:
      Two (02) copies of
  1. Completed filled application forms;
  2. Certified true copy of academic certificates, transcripts, birth certificate;
  3. Certified true copy of passport;
  4. Medical certificate issued by public medical hospitals certified that he/she is not suffering from any contagious illness or carrying a pandemic;
  5. Two recent passport size photographs, in colour, (with the name, surname and nationality of the candidate written on the back of the photos); and
  6. Applicant for Masters and PhD must provide a copy of an Abstract of dissertation/thesis of graduation/thesis for PhD degree.
     The scholarship will cover
(a)   (i) Monthly allowance of 750 Dirhams (Approximate to U.S $ 75);
(ii) Tuition fees;

(b)   Other costs will be covered by Applicant (Student)
(i)                 Accommodation;
(ii)              Registration fees; and
(iii)            Air ticket, go and return.
 
 Medical coverage:
Foreign students are required to subscribe to an insurance policy during their study stay in Morocco that offers them the following services:
      ·         Reimbursement of medical expenses;
      ·         Medical care;
      ·         Final medical evacuation to home country in cases of serious illness that will not allow           students to continue with their studies in Morocco; and
      ·         Repatriation of body in case of death in Moroccan territory.

For further information on the scholarships consult the websites: www.enssup.gov.ma  or www.men.gov.ma   or  www.ma2e.com  

Mode of Application 
The application shall be submitted in hard copy to reach the undersigned not later than 5th August, 2019 to:

Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,
P.O. Box 10,
40479 DODOMA
Room 404

TAARIFA KWA UMMA


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY

SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE PEOPLE’S DEMOCRATIC REPUBLIC OF ALGERIA FOR ACADEMIC YEAR 2019/2020

Call for Applications
The General Public is hereby informed that, the People’s Democratic Republic of Algeria  has granted a Scholarship programme to eligible Tanzanian Nationals to pursue Undergraduate studies at Universities in Algeria for the academic year 2019/2020 in the following field categories:

Category A. Higher Education
      1.      Medicine;
      2.      Technical Sciences;
      3.      Science of Matter;
      4.      Mathematics and Computer;
      5.      French;
      6.      Science of Nature and Life; and
      7.      Earth Science and the Universe.

Category B. Religious Affairs and Academic
1.         Imam preacher and/or Quran teacher;
2.         Bachelor degree (Licence) in Imamat.

Application Requirements
1.      Must have completed Advanced Secondary School or Diploma in 2017-2018;
2.      Will be not more than 25 years of age by October, 2019;
3.      Medical Examination Certificate from a Public Hospital; 
4.  Have a good knowledge of the Holy Quran for Imam Preacher/or Koran teacher applicants;
           5.    Have a good knowledge of the Holy Quran for Bachelor degree in Imamat 
            applicants.

Application Package
  §      Certified copies of;
-         Certificate of Secondary Education Examination (CSEE);
-         Certificate of Advanced Secondary Education Examination (ACSEE) or Diploma Certificates (Academic Certificates and Transcripts);
-         Birth Certificates;
  §      Application letter (with your contacts; telephone number and email address); and
     §    Medical Examination Certified by a Public Hospital;

NB:
     ·        Selected applicants will undergo one year for French language before commencing undergraduate degree studies.
     ·        There is no Loan or grant  from the Government of Tanzania  for candidates who will be offered this Scholarship.

Mode of Application
All applicants should submit their application packages to reach the undersigned  not later than 1630Hrs on 10th August 2019 to:

Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma (UDOM)
Business School,
Block 10,
40479 DODOMA.

Jumamosi, 20 Julai 2019

WAZIRI NDALICHAKO ATAKA USIMAMIZI THABITI UDAHILI WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa wito kwa Viongozi wa Elimu ya juu nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/20 ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wanafunzi, wazazi, walezi na wafadhili wa wanafunzi hao.

Waziri Ndalichako ametoa wito huo Jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho ya 14 ya elimu ya juu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi ambayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo Jukumu la Taasisi za Elimu ya Juu Katika Kuzalisha Ujuzi Unaohitajika kwa ajili ya Viwanda.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo ya programu zinazotolewa na Chuo Kikuu Dodoma wakati wa maonesho ya 14 ya elimu ya Juu yalivyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake amesema asingependa kuona changamoto zilizotokea mwaka jana katika kujiunga na vyuo zinajirudia kwani changamoto nyingine zilisababishwa na Vyuo vyenyewe kutokuwa na mifumo thabiti ambayo wanafunzi wangeweza kufanya maombi na kujithibitisha katika vyuo kwa urahisi.

“Nafahamu kwamba TCU wameshatoa mafunzo na maelekezo ya kutosha kwa wataalamu wa mifumo ya kompyuta na maafisa udahili wa vyuo vyote ambao mnadahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2019/20 kwa hiyo naamini kwamba zoezi la udahili kwa mwaka huu litafanyika kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka jana,” alisema Waziri Ndalichako.

Waziri Ndalichako  alisistiza kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu sura ya 346 ya sheria za Tanzania jukumu la kudahili wanafunzi ni la Seneti za Vyuo Vikuu au Bodi ya za Chuo husika, hivyo amewataka Viongozi wa Vyuo kutumia mamlaka ya Seneti za Vyuo Vikuu au Bodi kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu udahili wa wanafunzi ili waweze kujiunga kwa urahisi huku akisistiza pia  vigezo, masharti, taratibu na sifa za mwanafunzi kujiunga na chuo kuzingatiwa.

“Niwakumbushe tu  Serikali iko macho, katika mchakato wa udahili msipofuata taratibu mkaweka watu wasio kuwa na sifa tutawaondoa lakini kumbukeni na ninyi mloiwaingiza hamtabaki salama, hakikisheni zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi,”aliongeza Waziri Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo katika banda la DIT wakati wa maonesho ya 14 ya elimu ya Juu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam


Sambamba na hilo amewataka wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu kutokuwa wavivu wa kusoma maelekezo kabla ya kuanza kujiunga ama  kuchagua kozi katika vyuo. Amewaasa kuzingatia sifa zinazohitajika kwa kulinganisha ufaulu wao wakati wa kuchagua kozi huku akisistiza kuwa Serikali haina utaratibu wa kumpangia mwanafunzi programu ya kusoma isipokuwa inachagua mwanafunzi kutokana na sifa alizonazo katika kozi husika.

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu ya juu na Vyuo vikuu kuendelea kujitathmini ni kwa kiasi gani  tafiti ambazo wamekuwa wakizifanya zinagusa moja kwa moja jamii na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali  zilizopo katika jamii.

“Ninyi Taasisi za Elimu ya Juu macho yenu na masikio yawe wazi kila mara ili muweze kusikiliza wapi katiika jamii kuna changamoto na kwa kutumia utaalamu wenu mshiriki kuzitatua, kumbukeni elimu ya juu katika nchi yoyote ile ndio kitovu cha maarifa hivyo muendelee kutumika katika kutatua changamoto hizo,” aliongeza waziri Ndalichako.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kutembelea maonesho ya 14 ya elimu ya juu.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa maonesho Profesa Uswegi Minga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Tumaini amesema uwepo wa maonesho hayo umetoa nafasi ya vyuo vyenyewe kujitangaza kuhusu fursa zinazopatikana katika vyuo vyao, lakini pia imekuwa nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu  kutokana na kujifunza namna vyuo vingine vinavyofanya kazi hivyo kusaidia kufanya maboresho katika maeneo ya uendeshaji wa Vyuo lakini pia katika upangaji na ufundishaji wa programu mbalimbali.

Maonesho ya 14 ya Vyuo vya Elimu ya Juu yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini na kwa mwaka huu yamekuwa na washiri zaidi ya 80 vikiwemo kutoka nje ya nchi na vile vyaTanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akigawa cheti kwa moja ya Taasisi ambayo imeshiriki katika maonesho ya 14 ya elimu ya ju. Maonesho hayo yamefanyika  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Da res Salaam.

Ijumaa, 19 Julai 2019

TCU KUHAKIKISHA MITAALA KATIKA VYUO VIKUU INAANDAA WAHITIMU WANAOENDANA NA MATAKWA YA TAIFA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa (Mb) ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) nchini kuhakikisha mitaala inayotumika katika vyuo vikuu iweze kuandaa wahitimu siyo tu kwa kuajiriwa, bali pia kuwa na uwezo wa kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 14 ya elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia nchini ambapo amesema uwepo wa mitaala ya aina hiyo utasaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa ujumla.

“Nimeelezwa kuwa tayari baadhi ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu zimeshaanza kuchukua hatua za kutengeneza Mitaala mipya na kuhuisha ile ya zamani ili kuifanya iendane na mahitaji ya sasa ya taifa na soko la ajira, nitoe wito kwa Taasisi zote za Elimu ya Juu kuendelea kuhuisha na kuboresha mitaala yao kwa mwelekeo huo,” alisema Mhe Majaliwa.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) wakati alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ili kufungua maoesho ya 14 ya Elimu ya Juu Tanzania. 
Akizungumzia azma ya serikali ya kuongeza udahili katika Vyuo Vikuu, Waziri Mkuu ameitaka Tume ya Vikuu kutafuta mbinu za kuviwezesha vyuo zaidi ikiwa ni pamoja na kujengea uwezo vyuo vikuu binafsi ili visaidie katika kuongeza udahili pamoja na kufikia viwango vinavyotakiwa na siyo kuwapunguzia viwango vya matakwa ya usajili.

“Msimamo wa Serikali uko wazi na unataka Vyuo Vikuu Binafsi kuwa washirika muhimu kwenye maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Juu nchini, hata hivyo nai vema nikaeleweka vizuri hakuna mbadala wa elimu bora, ni wajibu wetu  kuhahakikisha vyuo vyote vinatoa elimu bora. TCU endeleeni kutekeleza majukumu yenu  ya kimsingi ya kudhibiti na kushauri lakini zaidi jipambanue  katika uwezeshaji wa vyuo hivyo ili kuondoa taswira hasi iliyojengeka katika jamii kuwa kazi ya Tume  ni kuvifungia vyuo vikuu badala ya kutatua changamoto zinazowakabili.” Alisema Mhe. Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akipata maelezo ya kazi zinazotekelezwa na Tume na Vyuo Vikuu nchini (TCU) kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Profesa Charles Kihampa. Taasisi hiyo ndio mratibu wa maoesho ya Taasisi ya Elimu ya Juu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
Alisema ili kuongeza idadi ya watanzania wanaopata nafasi ya Elimu ya Juu, ni lazima kama nchi kupanga mikakati kwa kushirikiana na sekta binafsi, ambao ni wadau wakubwa sana katika Elimu ya Juu kwani ukiangalia kati ya wahitimu wote wa Vyuo vikuu kwa mwaka, asilimia 25 wanatoka katika vyuo vikuu binafsi.

Katika hatua nyingine Mhe. Majaliwa ameitaka TCU kuhakikisha wanakutana na taasisi binafsi zinaowasaidia watanzania kupata nafasi katika vyuo vikuu nje ya nchi ili ziweze kuwatambua, kuwasajili lakini pia kufanya nao kazi kwa karibu ili kuwaambia mahitaji halisi ya kwenda vyuo vikuu ni yapi na wao washiriki katika kumshauri kijana ni alama zipi za ufaulu zinafaa kwenda kwenye digrii, diploma na ama cheti ili kuepukana na changamoto ya kutotambulika kwa vyeti pindi wanapohitimu katika ngazi hizo za elimu akitolea mfano watanzania ambao wamesoma kwenye moja ya Chuo Kikuu kilichopo nchini Misri lakini vyeti vyao kutotambulika.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa maoesho ya 14 ya Elimu ya Juu Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. 
 “Naona kundi kubwa la vijana wa kidato cha sita wanatafuta vyuo kupitia taasisi hizo ni vyema sasa TCU kwa kuwa mko katika maonesho hayo mshirikiane kuwasaidia vijana wetu hawa kupata vyuo vinavyostahiki ili wakienda kusoma akipata cheti na kurejea muweze kuvitambua vyeti hivyo,” alisema Mhe. Majaliwa

Awali Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha alimweleza Waziri Mkuu kuwa ili kuongeza idadi ya wahitimu watakaochochea ukuaji uchumi kwa kupitia sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi tayari baadhi ya vyuo vimefanya maboresho ya mitaala kutoka kwenye mfumo unaozingatia ufahamu na kwenda kwenye mfumo wa umahiri.

Pia Wizara kwa kushirikiana na Taasisi za sekta binafsi Tanzania imeanzisha mabaraza 6 ya kisekta ya ujuzi na maarifa katika Sekta za Kilimo, Ujenzi, Uchukuzi, Utalii, Nishati na TEHAMA kwa lengo la kushauri kuhusu mitaala na mahitaji halisi ya soko la ajira.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakati wa maoesho ya 14 ya Elimu ya Juu Tanzania yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Nae Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini Charles Kihampa amesema Maonesho ya Vyuo Vikuu kwa mwaka huu yamehudhuriwa na taasisi 81 ambapo taasisi 66 ni za ndani ya nchi na 15 ni taasisi za kutoka nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 14 ya elimu ya Juu Mwenyeketi wa Kamati ya Wakuu wa Vyuo vikuu vya Umma nchini Prof. Raphael Chibunda ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Serikali kwa Ujumla kwa kuhakikisha kuwa Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu inaongezeka jambo ambalo limepunguza migogoro katika Vyuo.

Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu yana kauli mbiu isemayo Jukumu la Taasisi za Elimu ya Juu katika kuzalisha Ujuzi unaohitajika kwa ajili ya Viwanda.
Mmoja wa watumishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akitoa ufafanuzi kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu Tanzania yanayofanyika jijini Dar es Salaam.