Alhamisi, 18 Juni 2020

SERIKALI KUTUMIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 KUWAENDELEZA WABUNIFU

Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 750 kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa ajili ya kuwaendeleza wabunifu 70 walioshiriki katika fainali za Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2020.


Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati akitangaza Washindi wa MAKISATU 2020 ambapo amesema Serikali imepanga kuendeleza ubunifu unaozalishwa ili kuwa bidhaa na kuchangia katika harakati za kukuza uchumi.


Waziri Ndalichako amefafanua kuwa MAKISATU ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuibua, kutambua na kuendeleza ubunifu na ugunduzi unaofanywa na watanzania hususani wa ngazi za chini.


Waziri Ndalichako ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadhamini wa MAKISATU 2020 ambao wamekuwa sehemu ya kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambao ni benki ya CRDB, VODACOM Foundation, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Binadamu (HDIF)







Maoni 2 :

  1. Hawa wanafunzi wapya wa kidato cha tano wanaanza lini masomo yao?

    JibuFuta
  2. Leo elimu ya Tanzania imeanza poteza watu mahili wa taaruma fulani kama ilivyo kuwa kabla kwa misingi mibovu ya chini kwa maono yangu tu. Mfano. Leo hii mwanafunzi anachukua taaluma ya biashara i.e EGM, ECA ,HGE n.k . akiwa na ndoto ya kuchukua faculties zinazo endana na anachokisomea . ila uko mbele yaani elimu ya juu inabomoa kama Leo hii BACHELOR OF ART IN ECONOMICS , ECONOMICS AND FINANCE etc . MTU wa HKL, HLF , HGL , HGK N.K anaweza pata nafasi umu wanafunzi wa biashara wakasome mini?

    Kwa upande wa afya bigup sana , viongozi wetu .

    JibuFuta